KOMBE LA MEYA SHINYANGA 2015 LAZINDULIWA,TIMU 18 KUCHUANA, MSHINDI KUONDOKA NA ZAWADI NONO!

No comments
Saturday, June 27, 2015 By danielmjema.blogspot.com

Mashindano ya Kombe la Meya Shinyanga 2015 (Pepsi Meya Cup 2015) yamezinduliwa rasmi leo na mkuu wa wilaya ya Shinyanga ndugu Josephine Matiro katika viwanja vya Shycom mjini Shinyanga.

Mashindano hayo ambayo yameandaliwa na mstahiki meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafidh Mukadam na kudhaminiwa na kampuni ya Vinywaji baridi ya  Pepsi (SBC Tanzania Ltd) yanashirikisha timu 17 za kata zote za manispaa hiyo na timu ya polisi Shinyanga.

Mashindano ya Kombe la Meya Shinyanga yakihusisha mpira wa miguu yataendelea kufanyika hadi tarehe 25,Julai 2015 na yatakuwa yanafanyika siku tatu kwa wiki yaani Ijumaa,Jumamosi na Jumapili.

Mshindi wa kwanza katika mashindano hayo ataondoka na kitita cha shilingi milioni moja na laki tano,kombe na medali ya dhahabu,wa pili shilingi milioni moja,kombe dogo na medali ya fedha na wa tatu shilingi laki tano,kombe dogo na medali ya shaba.

Malunde1 blog ilikuwepo wakati wa uzinduzi huo,Kadama Malunde,ametuletea picha kutoka eneo la tukio....

Mstahiki meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafidh Mukadam akizungumza wakati wa ufunguzi wa Pepsi Meya Cup Shinyanga 2015,ambapo alisema lengo la mashindano hayo ya mpira miguu kwa vijana yatakayoshirikisha timu 18 za manispaa ya Shinyanga ni kwa ajili ya burudani,ajira na kusaka vipaji kutoka kwa vijana katika manispaa ya Shinyanga.
Meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafidh alisema mashindano hayo yatakuwa yatafanyika kwa muda wa mwezi mmoja na yatafanyika mara tatu kwa wiki katika viwanja vitatu vya Shycom,Kambarage na Polisi mjini Shinyanga.
Mashindano hayo yameanza leo Juni 26,2015 yatafikia tamati Julai 25,2015

Hisani: Michuzi Media

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .