Kambi Mbwana achukua fomu ya ubunge Handeni Vijijini
Posted in
Breaking News
No comments
Friday, July 17, 2015
By
danielmjema.blogspot.com
Mwandishi wa Habari za Michezo na mdau wa maendeleo
ya wilaya ya Handeni, Kambi Mbwana, mwenye fulana ya CCM, akikabidhiwa
fomu ya kuwania Ubunge, Jimbo la Handeni Vijijini kwa tiketi ya Chama
Cha Mapinduzi (CCM) na Katibu Msaidizi wa CCM wilayani Handeni, Asha
Muya, wilayani Handeni, mkoani Tanga. Kulia kwa Mbwana ni Jerome
Mhando, mmoja wa wadau waliomsindikiza katika tukio la uchukuaji fomu
ya kuwania nafasi ya kuwatumikia wana Handeni. Picha na Mpiga Picha
Wetu.
Na Mwandishi Wetu, Handeni
MWANDISHI wa
habari za michezo na mdau wa maendeleo wilayani Handeni, mkoani Tanga,
amejitokeza rasmi katika mbio za kuwania ubunge jimbo la Handeni Vijijini kwa
kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Makabidhiano
hayo ya fomu yalifanyika mbele ya Katibu Msaidizi wa CCM wilayani Handeni, Asha
Muya, ikiwa ni siku chache baada ya milango ya uchukuaji fomu za kuwania nafasi
za Ubunge na udiwani kufunguliwa rasmi. Akizungumza
mara baada ya kuchukua fomu hiyo, Mbwana alisema kwamba ameamua kujitokeza
katika mbio hizo za ubunge ili afanyie kwa vitendo yale aliyokuwa anayapenda,
hususan katika suala zima la maendeleo, huku wachache wao wakishindwa kuelewa
faida ya harakati zake, zikiwapo zile za kuitangaza Handeni kwa njia
mbalimbali.
Alisema
wilaya yao imekuwa na changamoto kadhaa zinazohitaji nguvu za pamoja katika
suala zima la shida ya kubwa ya maji, migogoro ya ardhi, ukosefu wa huduma bora
za kijamii, hivyo kunahitajika jitihada na mipango ya pamoja kufanikishaji
mambo hayo.
“Nilikuwa
kimya kwa siku kadhaa nikiangalia akina nani wapo katika mchakato wa kuhitaji
nafasi ya kuwatumikia wananchi wa Handeni Vijijini na kusikitishwa na watu
wasioishi huku na wasiokuwa na uchungu wala dhamira ya kuwakwamua
wananchi wakijitokeza
kwa wingi kuwania nafasi ya ubunge, inaonyesha wapo kwa maslahi yao
zaidi.
“Hii haiwezi
kukubalika, ukizingatia kwamba wananchi wameendelea kuishi maisha ya mashaka
kwa kukosa maji safi, elimu, afya, michezo, utamaduni na mambo mengine
yanayopaswa kufanyiwa kazi kwa kushirikiana na watu wote, wakiwamo viongozi wa
kisiasa, watendaji wa serikali na Watanzania kwa ujumla,” alisema
Mbwana.
Licha ya
kuonekana mpya katika ulingo wa kisiasa hususan kwa nafasi ya ubunge, Mbwana
anakumbukwa na kushukuriwa na wengi kutokana na mradi wake wa Tamasha la
Handeni Kwetu linalofanyika kila mwisho wa mwaka, kuasisi Taasisi ya Handeni
Kwetu Foundation, bila kusahau kuandika kitabu kinachojulikana kama Dira na
Tumaini Jipya Handeni kilichopokewa kwa hisia tofauti, haswa kutokana na
kilichoandikwa kwenye kitabu hicho.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :