Kichupa cha 'Utanipenda' cha Diamond nyuma ya pazia
Posted in
Habari na Jicho Pevu la Kijiwe
No comments
Saturday, December 19, 2015
By
danielmjema.blogspot.com
Nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ akiwa kasimama mbele ya magari aliyoyatumia katika video yake mpya ya Utanipenda.
Staa wa Bongo, Jacqueline Wolper, akiongea jambo na Diamond.
Gari ya Wolper katika video hiyo ikimmwagia maji Diamond.
Diamond akiangalia vipande vya video hivyo kabla ya kuendelea kushuti.
Diamond akiangalia Magazeti Pendwa baada ya kupata matatizo, nayo hayakuwa nyuma kuandika.
Diamond akipiga kinanda huku akimuimbia mpenzi wake Zari.
Mama yake Diamond, Sanura Kasim (kushoto) akifukuzwa na mlinzi baada ya kwenda kuomba msaada kwa JK.
Diamond akiongea jambo.
Sasa hivi kwenye ulimwengu wa muziki, gumzo ni ngoma aliyoitoa Mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’ inayokwenda kwa jina la Utanipenda.
Ni ngoma kali ambayo itatambulishwa kwa mara ya kwanza ndani ya Ukumbi wa Kimataifa wa Burudani wa Dar Live uliopo Mbagala jijini Dar.
Mbali na utambulisho wa ngoma hii ambayo itapigwa live kwa kutumia vyombo, nyimbo nyingine ambazo Diamond atazipiga siku hiyo ni pamoja na Mdogomdogo, Nasema Nawe, Nana na nyinginezo zinazobamba huku akiwa na madansa wake kutoka Wasafi Classic Baby (WCB). Itakuwa ni siku ya Krismasi (Ijumaaa ijayo) ambayo msanii huyo ameahidi kufanya mambo makubwa akisindikizwa na mkali wa nyimbo za Singeli, Msaga Sumu pamoja na wacheza dansi hatari Afrika Mashariki, Wakali Dancers na wasanii wengine kibao. Burudani yote hiyo ambayo imedhaminiwa na huduma kutoka kampuni ya simu Tanzania, Airtel Money utaipata kwa kiingilio cha shilingi 15,000 tu getini na wale watakaohitaji huduma ya VIP watalipia shilingi 30,000.
Katika kuelekea kwenye shoo hiyo, Showbiz ilifanikiwa kunasa baadhi ya picha za nyuma ya pazia ‘behind the scene’ wakati kichupa cha wimbo huo kikiandaliwa. Video hiyo ni mkono wa yuleyule mkali wa vichupa kutoa Sauzi anayekwenda kwa jina la God Father.
Hajakosea! Amefanya bonge la kazi na hata mashabiki ni mashahidi kwamba wimbo ni mkali na kideo chenyewe ni ‘kitamu’. Maneno mengi siyo ishu, kwenye hili picha zinaongea zaidi hivyo pitisha macho kwenye baadhi ya picha hizo ili upate uhondo! Kwani kuna mtu kaibiwa? Imeandaliwa na Andrew Carlos/GPL
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :