KENYA: SIMBA WATOROKA MBUGANI NA KUINGIA MITAANI NAIROBI
Posted in
afrika mashariki
No comments
Friday, February 19, 2016
By
danielmjema.blogspot.com

Shirika hilo limewataka wakaazi wa maeneo hayo kutahadhari. Hii si mara ya kwanza kwa wanyama hao kuzua taharuki katika eneo hilo.
Msemaji wa Shirika hilo Paul Udoto ameambia BBC nchini Kenya kwamba wamepokea habari kwamba simba hao wa kike walionekana katika nyumba za NHC katika eneo la Langata na mitaa mengine inayopakana na Barabara ya kusini.
''Haya ni maeneo ambayo yana watu wengi, na hii ndio maana tumeimarisha msako wetu,'' aliambia BBC kwa njia ya simu, yeyote aliye na habari kuwahusu anapaswa kutoa habari hizo mara moja.
Langata ni eneo lililo na watu wengi na maafisa wa KWS pamoja na polisi wanahofia kwamba wanyama hao huenda wakasababisha hasara iwapo hawatapatikana haraka na kurudishwa katika mbuga hiyo.
Simba sita waliripotiwa kutoroka katika mbuga hiyo Alhamisi jioni lakini wanne kati yao walipatikana .
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :