Wapiganaji takriban 100 wa kundi la kigaidi la Alshabab wamevamia kituo kimoja cha polisi Wajir Kaskazini mwa Kenya. Hadi
kufikia sasa idadi ya waliojeruhiwa ama kufa haijajulikana lakini
kinachothibitishwa na serikali kuwa walifaulu kuteka gari la serikali
aina ya Land Cruiser.
''wavamizi walishambulia kituo cha polisi
cha Diff na wakakabiliwa vikali na askari waliokuwepo, wengi wao
walijeruhiwa ila walifaulu kuteka nyara gari la serikali la kituo cha
Diff ambalo walitumia kuwabeba majeruhi wao'' alisema Inspekta Jenerali
wa polisi wa Kenya Joseph Boinnet.
Maafisa 3 wa polisi wa Kenya walijeruhiwa. Kundi hilo lilitorokea mpakani. Kikosi cha jeshi la Kenya limewafuata huko baada yao kuvuka mpaka kati ya Kenya na Somalia.

No comments:
Post a Comment