Kumekuwa na theory nyingi mitaani kuwa watu wenye intelligence kubwa
na ma-genius wengi wana tabia nyingi za ukichaa au ni vichaa kabisa,
madaktari bingwa wengi kwenye mahospitali makubwa hapa nchini ambao
wanategemewa wengi huwa ni "wehu".
Hata katika viunga vya vyuo vikuu maprofessor wengi wakubwa wa kuaminika wengi huwa ukikaa nao utagundua tu wana-"wehu" fulani. Ukifuatilia biography nyingi za watu waliokuwa na uwezo mkubwa wa
kiakili na wavumbuzi wengi wakubwa hapa duniani katika sayansi na katika
sanaa utagundua historia zao zimegubikwa na uchaa wa hali ya juu.
Mtu kama Isaak Newton inasemekana alikua na magonjwa ya akili na
saikolojia ambayo kwa sasa kitaalamu yanaitwa "schizophrenia", huu ni
ugonjwa wa mtu kutokuweza kuishi na mtu yeyote,historia inaonesha Newton
alikuwa ni mtu wa kujistukia muda wote kama mtu aliyeua vile, na mara
nyingi aliwashutumu ndugu zake kuwa wanataka kumuwekea sumu kwenye
chakula. Alipofika miaka 40 hali ilikua mbaya zaidi na alikua hawezi
kuishi hata na ndugu zake wa karibu akajitenga completely.
Albeit
Einstein yeye alikua na tabia ya uchafu uliopindukia, inasemekana chumba
alichokuwa akiishi kilikua kama zizi la nguruwe, kula hapo hapo
kujisaidia hapo hapo hakuna mtu wakawaida anayeweza kuingia ndani,
kilikua kinanuka kwa uvundo lakini pia hata nguo zake alikuwa anaweza
kuvaa miezi bila kufua na kutokana na tabia yake ya uchafu na
kutokujipenda na kutopenda kunyoa wengi walijua ni mwehu, wataalamu wa
magonjwa ya akili kwa sasa wanauita ugonjwa huu schizotype.
Alexander
Graham Bell, huyu ni mvumbuzi wa simu, yeye alikua na tatizo la hisia
kali za mapenzi , hisia zilizopitiliza mpaka alikuwa kero kwa mpenzi
wake miss Hello.
Inasemekana alikua kama zombi kabisa kwa mpenzi wake
kuna nyakati ilibidi mpenzi wake huyu amkimbie, lakini pamoja na
kumkimbia huku siku alipovumbua tu simu neno la kwanza katika simu
lilikua ni kutaja jina la mpenzi wake HELLO na hapo ndio utamaduni wa
kuanza na neno HELLO kwenye simu ulipoanzia, japo watu wa kizazi hiki
wanachukulia kama ni fashion lakini neno HELLO lilitajwa na mtu
aliyekuwa na emotion breakdown wakati huu.
Martin Luther huyu alikua na
tatizo la misongo ya mawazao iliyotukuka (chronical depression), lakini
pia alikua ni mtu mwenye "mizuka ya ajabu, siku akiamka kichwa kimemtuma
kufanya kazi anaeza fanya kazi hata 48 hrs non-stop, siku kichwa
kikimtuma kusoma anaweza kusoma hata 36 hrs non-stop.
Mwaka 1517 kichwa
kilimtuma kuandika Thesis za kupinga namna Kanisa Katoliki
linavyoendeshwa, aliandika thesis 95 alipoona hawamuelewi akaamua
kuzibandika mlangoni mwa kanisa la Wittenberg halafu akasepa, na hapo
ndipo ikaanza movement ya protestant churches.
Wapo wengi kama Thomas Edson, Leonardo da Vinci, Michelangelo
Buonarroti, Theodore Roosevelt,John Nash,Michael Faraday, Henry Ford na
wengine kibao ambao historia zao zinapatikana kiurahisi, wote hawa
wameonesha kuwa na degree fulani ya ukichaa ambayo ni tofauti na mtu wa
kawaida kama ambavyo sayansi ina-define na wengi wamekuwa na tabia ya
kuongea wenyewe muda wote.
Kuna vitabu vimeandika research ya hii kitu na
wakafanya clinical trials wakagundua kuwa asilimia kubwa za watu wenye
akili nyingi au ma-genius familia zao pia kuna vichaa wengi au watu
wenye upungufu wa akili au wehu.
Moja ya kitabu kizuri ni cha mwanamama Nancy C. Andreasen, M.D., Ph.D.
kinaitwa "The Creating BRAIN, Neurosciences of Geinus" kimejaribu sana
kutafiti kwa kutumia technolojia nzuri ya MRI bongo nyingi za ma-genius
na kimegundua zinafanana neuro-arrangement zake na kua sehemu za brain
zao haziko developed kabisa.
Swali hapa linakuja je kuna uhusiano gani kati ya kuwa na Intelligence kubwa au kuwa genius au kuwa highly creative na UKICHAA??

No comments:
Post a Comment