Muitaliano Antonio Conte anakabiliwa na kazi kubwa wakati akichukua
mikoba katika klabu ya Cheslea msimu ujao. Hayo ni maneno ya kaimu kocha
wa Guus Hiddink.
Kazi yake itakuwa ni kuwarejesha mabingwa hao wa msimu uliopita kileleni mwa Premier League baada ya kuwa na msimu mbovu. Hiddink anahisi kuwa kikosi hicho cha Chelsea inakosa wachezaji ambao wanaweza kutegemewa katika kutoa mwongozo wa mafanikio kama ilivyokuwa katika muongo mmoja uliopita.
Hiddink alikutana na Conte Jumatatu wiki hii baada ya kocha huyo mtarajiwa kuzuru uwanja wa mazoezi wa Chelsea ili kujifahamisha na mazingira yake mapya.

No comments:
Post a Comment