MAPATO YA BILIONI 400 KUPOTEA IMEFANYA RAIS WA TANZANIA, DKT. JOHN MAGUFULI AVUNJE BODI YA MAMLAKA YA MAWASILIANO NA KUMSIMAMISHA MKURUGENZI WAKE.
Posted in
afrika mashariki
No comments
Wednesday, April 27, 2016
By
danielmjema.blogspot.com
Kufuatia upotevu wa mapato, takribani shilingi bilioni 400 Rais wa Tanzania, Dkt. John katika mamlaka ya mawasiliano (TCRA), Rais wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amechukua maamuzi magumu ya kuivunja Bodi ya mamlaka hiyo na kumsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Dkt. Ally Yahaya Simba kutokana na kutosimamia ipasavyo mkataba wa utekelezaji wa mfumo wa usimamizi wa mawasiliano ya simu (TTMS).
Rais Magufuli amechukua hatua hiyo jana tarehe 26 April 2016 Ikulu Jijini Dar es salaam baada ya kufanya kikao cha kazi kati yake na viongozi na wataalamu kutoka Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Wizara ya fedha na Mipango na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).
Tarehe 22 Machi, 2013 Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) iliingia mkataba na kampuni ya SGS juu ya uwekaji, uendeshaji na uhamishaji wa mapato ya simu ambapo kampuni hiyo ilipaswa kutekeleza vipengele vitano lakini mpaka sasa kampuni ya SGS haijaanza kutekeleza kipengele kidogo kinachohusiana na uthibiti wa mapato ya simu za ndani (Offnet), hali ambayo imesababisha serikali kukosa mapato yanayokadiriwa kuwa shilingi bilioni 400 kwa mwaka.
Pamoja na kuivunja bodi ya TCRA inayoongozwa na Profesa Haji Semboja na Kumsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Dkt. Ally Yahaya Simba, Rais Magufuli pia amemuagiza Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa Mnyaa kumteua Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo mara moja.
Aidha, Rais Magufuli amewataka Waziri Prof. Mbarawa, Katibu Mkuu na Naibu Katibu katika wizara hiyo kuchukua hatua mara moja ili mfumo wa ukusanyaji wa mapato ya simu kwa simu za ndani (Offnet) uanze kufanya kazi na nchi ipate mapato yanayostahili kukusanywa.
“Waziri hakikisha unachukua hatua mara moja, nataka tukusanye mapato yote ya serikali yanayostahili na sitosita kuchukua hatua dhidi ya yoyote atakayekwamisha jambo hili” Amesisitiza Rais Magufuli.
Taarifa imetolewa na IKULU ya Tanzania-Dar es salaam.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :