MFAHAMU MWANAHARAKATI DEDAN KIMATHI WACIURI (Oktoba 31, 1920 - Februari 18, 1957),

No comments
Thursday, April 28, 2016 By danielmjema.blogspot.com

UKIAMBIWA utaje angalau majina ya wazalendo 10 wa Afrika waliojitolea kupigania uhuru wa Waafrika wenzao kutokana na manyanyaso na ukandamizaji wa makaburu wakoloni, baada ya majina kama vile, Nelson Mandela, Jomo Kenyatta na Julius Nyerere, jina la Mwanamapinduzi, Dedan Kimathi Waciuri (Oktoba 31, 1920 - Februari 18, 1957), haliwezi kosekana.


Alizaliwa katika Kijiji cha Thenge, Tarafa ya Tetu, Wilaya ya Nyeri. Akiwa na umri wa miaka 15, Kimathi alijiingiza katika uanaharakati, kwa kujiunga na kundi la waasi wafrika waliokuwa wanapinga utawala wa makaburu.

Kimathi kwa bahati hakushudia matunda ya kile alichopigania kwani alikamatwa na kuhukumiwa kunyongwa hadi kufa na utawala wa makaburu wa Uingereza waliokuwa wakiitawala Kenya. 


Inadaiwa kuwa wakoloni walikuwa wanamchukulia Kimathi kama Gaidi lakini Wakikuyu wengi (Wakenya) walikuwa wanamuona Kimathi kama mtetezi wa wanyonge na mpigani uhuru kwa maslahi ya vizazi vijavyo hivyo kwao alikuwa ni mkombozi na kiongozi wa vuguvugu la Mau Mau.


Kimathi alianza elimu yake katika shule ya msingi Karuna-ini, ambapo alijitahidi kuboresha uwezo wake wa kuzungumza lugha ya Kiingereza. baadae Kimathi akiwa na uwezo wa kuzungumza kiingereza kwa ufasaha, alijiunga na shule ya upili Tumutumu, kwa ajili ya elimu ya Sekondari lakini kwa bahati mbaya aliamua kuacha kutokana na kukosa Ada.

Katika maisha yake, Kimathi hakuwa ni mtu wa bahati kwani alijitahidi kutafuta kazi bila mafanikio kabla ya kuamua kujiunga na Jeshi kwa ajili ya Vita vya Dunia vya pili (1941) lakini nako mambo hayakumuendea vizuri kwani Mwaka 1944, alifukuzwa Jeshini kutokana na utovu wa nidhamu.

Mwaka 1946, Alijiunga na Kenya African Union. Mwaka 1949, alianza kufundisha katika shule yake ya zamani, Tumutumu lakini aliacha miaka miwili baadae.


 Vuguvugu la Mau Mau 

Licha ya kutodumu kazini katika kila ajira lililokuja mbele yake, Dedan Kimathi alifanikiwa kuwashawishi aliokutana nao kazini ambapo mwaka 1950, alijikuta akijikita katika siasa ambapo moja ya mambo aliyoyafanya ni kujiunga na vuguvugu la Mau Mau, akala kiapo na kujiunga kundi la watu 40, lililojulikana kama Kikuyu Central Association (1951), walioingia msituni kupambana na makaburu.

Mwaka 1956, Kimathi alikamatwa akiwa pamoja na mmoja wa wake zake (Wambui) na kuhukumiwa kuuwawa na mahakama ya kikaburu, iliyoongozwa na Jaji mkuu wa wakati huo,  Sir Kenneth O'Connor, akiwa amelazwa Hospitalini katika Hospitali ya General Hospital Nyeri. Februari 18, 1957 majira ya Alfajiri alinyongwa. zoezi hilo lilifanyika katika Gereza la Kamiti Maximum Security Prison.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .