Sunday, April 17, 2016

TUNDAMAN ANUSURIKA KIFO AJALINI HUKO IDETELO

Mwanamuziki wa Bongo Flava, Tunda Man leo amenusirika kifo baada ya kupata ajali mbaya eneo la Idetelo, katikati ya Nyololo la Makambako, nchini Tanzania



Kwa mujibu wa Tunda Man  akiwa amesinzia ghafla alisikia mlio mkubwa uliopelekea gari yao kupoteza muelekeo na kuelekea porini, ndani ya gari yao kulikuwana watu watano ambao mmoja wao alifariki dunia papo hapo huku wengine wakijeruhiwa.

Aidha Tunda Man amemtaja marehemu kuwa ni  Mussa maarufu kwa jina la Man Katuzo ambaye taratibu za kusafirisha mwili wake kuupeleka Kilosa mkoni Morogoro zinaendelea.

Source:  GPL

No comments:

Post a Comment