UHURU AWAFUNIKA MARAIS WA UKANDA WA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA UTAJIRI

No comments
Wednesday, April 27, 2016 By danielmjema.blogspot.com



RAIS wa Kenya, Uhuru Kenyatta ametajwa kuwa Rais Tajri zaidi na mwenye nguvu kubwa kiuchumi, katika ukanda wa Afrika mashariki ambapo utajiri wake unatajwa kuwa juu zaidi ya marais wote katika nchi zilizopo kusini mwa Jangwa la Sahara, zikiwemo Tanzania, Uganda na nchi jirani za Rwanda, Burundi, Msumbuji na hata Zambia.


Hayo ni kwa mujibu wa Jarida maarufu la Forbes ambapo kwa Afrika, Uhuru anashika nafasi ya 26, lakini kwa Kenya na Afrika Mashariki, ndiye kinara kutokana na kuwa na utajiri unaokadiriwa kuwa na thamani ya dola za Kimarekani milioni 600 (sh bilioni 463 za Kenya).


Uhuru, ana utitiri wa biashara na ardhi ya kutosha ndani ya Kenya. Anatajwa kuwa na zaidi ya ekari 500,000 ndani ya Kenya, akirithi ardhi iliyotwaliwa na baba yake katika miaka ya 1960 na 1970.

Anamiliki kiwanda kikubwa cha bidhaa za maziwa cha Brookside Dairies, kituo maarufu cha televisheni cha K24, benki na hisa katika moja ya mashirika makubwa ya ndege nchini humo, achilia mbali biashara nyingine kubwakubwa za ndani na nje ya Kenya.

Nafasi ya pili katika ukanda wa Afrika mashariki na kati na nafasi ya 31 barani Afrika, yupo Mkurugenzi mkuu wa Centum Investment, Chris Kirubi, inayomiliki Nation Media Group, Standard Chartered Kenya na Kenya Commercial Bank Group. Kirubi amefanikiwa kukusanya utajiri wa dola milioni 300, sawa na takribani Sh bilioni 220 za Kenya 

Kwa mujibu wa Jarida la Forbes, Mfanyabiashara wa Nigeria, Aliko Dangote ndiye anayeoongoza kwa Utajiri barani Afrika ambapo anashika nafasi ya 51 duniani akiwa na utajiri unaokadiriwa kufikia dolla bilioni 15.4.

Utajiri wake ni mara mbili ya mmiliki wa Chelsea Roman Abramovich ambaye anashika nafasi ya 137 Duniani. Dangote alizaliwa kwenye familia ya wafanyabiashara katika jiji la Kano ambalo ni la pili kwa ukubwa nchini Nigeria. Akiwa na umri wa miaka 21, mjomba wake akampa mkopo wa kuanzisha biashara yake mwenyewe.

Bwana Dangote ameorodheshwa tajiri wa 51 Duniani ukilinganisha na nafasi ya 67 mwaka 2015 wakati gazeti hilo la Forbes lilipoiweka mali yake kufikia dola bilioni 14.7.



Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .