Muungano wa Upinzani Kenya (CORD) wanaandamana kuipinga IEBC

Posted in
No comments
Monday, May 23, 2016 By danielmjema.blogspot.com

Muungano wa upinzani nchini Kenya CORD unafanya maandamano katika miji mikuu nchini humo kuwashinikiza maafisa wakuu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (IEBC) kujiuzulu.
Viongozi wa muungano huo wamesema maafisa hao hawawezi kuandaa uchaguzi huru na wa haki mwaka ujao. Polisi walitumia mabomu ya kutoa machozi na marungu kutawanya maandamano sawa na hayo Jumatatu wiki iliyopita.
Mashirika ya kutetea haki za kibinadamu walisema polisi walitumia nguvu kupita kiasi wakati wa maandamano hayo. Taarifa kutoka mji wa Mombasa zinasema polisi tayari wametumia mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya waandamanaji.
Mtu aliyeshuhudia amenukuliwa na shirika la habari la Reuters akisema polisi wa kukabiliana na fujo wamekuwa wakishika doria katika barabara za mji huo. Maduka mengi yamefungwa kutokana na wasiwasi wa kuzuka kwa fujo na kutokea kwa uporaji.
Awali Kiongozi mwenza wa mrengo wa CORD, Moses Wetangula amewahusisha Wabunge watatu kutoka mrengo wa Jubilee na jaribio la kuvuruga maandamano ya amani yanayofanyika leo, mjini Jijini Nairobi kupinga uwepo wa maafisa wa IEBC ofisini.
Wetangula alimtuhumu Mbunge wa Starehe, Maina Kamanda, Moses Kuria (Gatundu South) na Mbunge wa Dagoretti kusini, Dennis Waweru ambao wanafanya kazi chini ya mwavuli wa GEMA, akidai wamekuwa wakiuhamasisha umma na vijana wakorofi kuvuruga maandamano yao.
Wetangula alisema kuwa Wabunge hao pia wamekuwa wakiwatumia vijana hao (Hooligans), kuwarushia mawe ambapo katika maandamano yaliyopita ni wao waliohusiska kusababisha vurugu.
“Hatujihusishi na Siasa za ukabila ambayo kwa sasa zinatumiwa na watu wa Jubilee, ambao wanajiita GEMA, tunahisi kuwa serikali inahusika pia katika mipango ya hawa watu (wabunge) kuvuruga maandamano yetu ili tuonekana tunapenda fujo," alisema
Kiongozi huyo wa Ford Kenya, alisema maandamano yao yamekuwa ya amani ukiacha matukio machache ya vijana waliokodiwa kuingilia maandamano na kusababisha vurugu.
"Leo kutakuwa na maandamano ya aina hiyo katika miji ya Mombasa, Kakamega na Bungoma kuonesha uzito wa madai yao dhidi ya IEBC, tumewajulisha Polisikabla ya kuanza kuwa tutakuwa na maandamano kila Jumatatu kwa hiyo wanapaswa kutulinda na sio kutupiga na Teargas," alisema Wetangula.  

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .