Tanzania inaongoza kwa kuwa na watu wasiowaaminifu (Dishonest)
Posted in
afrika mashariki
No comments
Monday, May 16, 2016
By
danielmjema.blogspot.com
Utafiti umefanywa na wanafunzi wa University of Nottingham Uingereza ukihusisha nchi 159, wanafunzi wa chuo kikuu cha Nottingham wamefanya utafiti wa kugundua ni nchi zipi zinaoongoza kwa uaminifu au ukweli duniani, utafiti umefanywa ukihusisha nchi 159 ikiwemo Tanzania.
Wanafunzi hao wamefanya tafiti huku wakichanganya na data za 2003 za ukwepaji kodi, rushwa na udanganyifu katika siasa lakini wamegundua kuwa nchi za Lithuania, Uholanzi, Uingereza, Sweden, Ujerumani na Italia zimetajwa katika list ya nchi zinazoongoza kwa uaminifu.
Wakati nchi za Tanzania, China, Uturuki, Poland na Morocco zimetajwa kuwa ni miongoni mwa nchi zinazoongoza watu wake kutokuwa waaminifu, utafiti huo unaeleza kuwa watu wanaoishi katika nchi zenye rushwa na siasa za udanganyifu wamekuwa sio waaminifu au wakweli, wakati watu wanaotokea katika nchi ambazo hazina rushwa na ukwepaji kodi ni waaminifu.
Tafiti zimefanyika katika chuo kikuu cha Nottingham Uingereza, lakini kimetajwa kufanya majaribio kwa kuhusisha vijana 2,586 wenye wastani wa umri wa miaka 22 kutoka nchi 23 zikiwemo Vietnam, Morocco, China, UK, Hispania, Sweden, Italy na Czech Republic. Utafiti huu umetolewa na dailyamail.co.uk March 11 2016.
IMEANDIKWA : dailymail.co.uk
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :