Jivu la aliyekuwa rais wa Cuba Fidel
Castro limezikwa katika kiunga cha makaburi mjini Santiago, na hivyo
kumaliza siku tisa za maombolezo ya kitaifa nchini Cuba.
Hapo jana, rais wa Cuba, Raul Castro, amesema serikali yake itakataza barabara au eneo lolote kupewa jina la Fidel, na ndivyo Fidel mwenyewe alivyoagiza.
Mbele ya mhadhara mkubwa mjini Santiago, alisema Fidel Castro hakutaka kufanywa kama kiongozi wa madhehebu.

No comments:
Post a Comment