HIVI ULISIKIA ILE STORI KWAMBA WACHEZAJI WA TWIGA STARS WANASHIRIKI MAPENZI YA JINSIA MOJA? UPANDE WA PILI NDIO HUU….
Posted in
No comments
Wednesday, June 27, 2012
By
danielmjema.blogspot.com
.
Vyombo mbalimbali vya habari
vya Tanzania likiwemo gazeti la Mwananchi vimenukuliwa vikiripoti stori
kwamba Kocha wa timu ya taifa ya Twiga Stars aliejiuzulu Boniface Mkwasa
alisema moja kati ya mambo yaliyomkera Twiga Stars ni wachezaji kadhaa
kushiriki katika mapenzi ya jinsia moja, wao kwa wao kwenye timu.
Exclusive on millardayo.com
Nahodha wa timu hiyo Sophia Mwasikili amesema “nimefurahi kulizungumzia
hilo swala kwa sababu limekua likizungumzwa kwenye magazeti mengi bila
uthibitisho, kocha hakuzungumza kwamba kuna vitendo kama hivyo alisema
vilikuepo kipindi cha nyumba lakini kwa sasa havipo, nimekua Twiga Stars
toka 2006 mpaka sasa sijaviona hivyo vitendo labda mwalimu ndio aliona
kwa mchezaji lakini hakuna yeyote ambae amewahi kuripoti kwangu”
“Wazazi wetu hawajapenda hili
swala, tumedhalilishwa na hata kama kuna mchezaji alifukuzwa kutokana na
hilo basi itakua ni siri kati yake na mwalimu hatujawahi kuambiwa, kama
Mkwasa atapatikana ni vizuri amtaje huyo mtu il iwatanzania wajue
lakini kiukweli hakuna vitendo kama hivyo Twiga Stars” – Sophia
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :