Marekani Yataja Makundi Hatari Afrika
Posted in
No comments
Wednesday, June 27, 2012
By
danielmjema.blogspot.com
Makundi
matatu ya kigaidi Barani Afrika yameanza kushirikiana katika harakati
zao. Hii ni kwa mujibu wa Mkuu wa jeshi la Marekani anayesimamia
shughuli za usalama kanda ya Afrika. Jenerali Cater Ham amesema kundi la
Al Qaeda Afrika Kaskazini limekuwa likiwasaidia wanachama wa Boko Haram
nchini Nigeria na mabomu.
Akizungumza
mjini Washington afisa huyo amesema waasi wanaodhibiti kaskazini mwa
Mali wameendelea kutumia eneo hilo kuendesha harakati zao ikiwemo
kupanga njama za kutekeleza mashambulio.Jenerali Ham ni kamanda wa
kitengo cha idara ya ulinzi ya marekani kinachofuatilia masuala ya
usalama barani Afrika{Africom} na makao makuu yako Ujerumani.
Kitengo
hiki kinaimrisha harakati zozote za kijeshi Afrika ikiwemo mashambulio
ya kutumia ndege bila rubani dhidi ya wapiganaji wa Kisomali wa Al
shabaab.
Tayari
kuna wanajeshi 100 wa Marekani wanaosaidia kumsaka kiongozi wa waasi
Uganda Joseph Kony ambao wanasimamiwa na kitengo cha Jenerali Ham.
Afisa huyo ametaja makundi hatari zaidi ikiwa ni pamoja na kundi la Al Qaeda Afrika Kaskazini{AQIM}, Boko Haram na Al-Shabab.
Ameongeza tisho kubwa ni kwamba makundi haya yameanza kushirikiana katika kufanikisha harakati zao.
Mapema
mwaka huu nchi ya Mali ilishuhudia mapinduzi ya kijeshi na kufuatiwa na
kudhibitiwa kwa eneo nzima la Kaskazini na makundi yanayotetea
kujitenga ya Tuareg na wapiganaji wa kiisilamu.
Chanzo: http://www.bbc.co.uk/swahi
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :