klabu ya Mout Kilimanjaro Marathon 1991 yaanzisha mbio za “Great Kilimanjaro Run – GKR”
Posted in
No comments
Wednesday, June 27, 2012
By
danielmjema.blogspot.com
Baada
ya mafanikio makubwa ya kumleta mcheza sinema maarufu wa Marekani
Deidre Lorenz kushiriki mbio za Mount Kilimanjaro Marathon zilizotimua
vumbi tarehe 24 Juni 2012 sasa klabu ya Mout Kilimanjaro Marathon 1991
imeanzisha mbio za “Great Kilimanjaro Run – GKR”
GKR
zitafanyika mjini Moshi kila mwaka kuanzia tarehe 22 - 28 October 2012
zikishirikisha klabu zote za riadha kutoka mkoa wa Kili manjaro. GKR
itazishikisha mbio fupi (Track and Field events) na kumalizia na
marathon siku ya jumapili tarehe 28 October.
Akizungunzia
uamuzi wa kushirikisha mbio fupi katika GKR Rais wa klabu ya Mt.
Kilimanbjaro Marathon 1991 Onesmo Ngowi alisema kuwa klabu yake inataka
kuziendeleza pia mbio fupi na michezo mingine ya uwanjani badala ya
kuweka juhudi zote kwenye marathon tu.“Watu wamekazania sana marathon na
kusahau mbio fupi ambazo zilishawahi kuliletea taifa hili sfa kubwa
sana” alisema Ngowi kwa msisitizo.
Kuanzishwa
kwa GKR kutaufanya mji wa Moshi kuwa na mbio tatu za marathon kwa sasa
na hii inaufanya mji huu kutoa nafasi kubwa kwa wanariadha kukuza na
kuendeleza vipaji vyao.
Tutamleta Haile Gabreselasie aje kuzindua mbio hizi” alisema Ngowi
ambaye mwaka jana alikuwa na mazungumzo marefu jijini Addis Ababa na
gwiji hili la mbio ndefu duniani kutoka nchi ya Ethiopia. Ngoiwi aliweza
pia kutiliana mkataba na shirika la ndege la Ethiopia (Ethiopia
Airlines) jijini Addis Ababa kufadhili mbio za Mount Kilimanjaro
Marathon. Kwa sasa Ethiopia Airlines (ET) ndio wafadhali pekee wa Mount
Kilimanjaro Marathon. ET wanatoa punguzo kwa wakimbiaji wanaoshirtiki
kwenye mbio hizi kutoka sehemu mbalimbai duniani.
Aidha,
ET wanalipia gharama za kutangaza mbio hizi wakati wa New York
Marathon, L.A Marathon na Boston Marathon. Hii inaitangaza sana Tanzania
kwani mbio hizi tatu zinawashirikisha wakimbiaji wengi sana kutoka
katika nchi nyingi duniani. Kwenye mbio hizi za Marakani Mt. Kilimanjaro
Marathon huweka banda la maonyesho linaloitangaza Tanzania na vivutio
vyake.
Pia
Mt. Kilimanjaro Marathom huchezesha nahati nasibu (raffle) kwenye mbio
hizi tatu za Marekani ili kuwapata washiriki maarufu kama Deidre Lorenz
kuja kukimbia na kuitangaza vyema Tanzania.
Aliendelea
kusema kuwa nchi hii ni yetu sote hivyo tuna jukumu la kuitangaza na
kuiendeleza wote alisisitiza Ngowi ambaye mwaka 2000 ofisi ya Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilimpa tuzo ya “Mwanateknolojia wa Karne
ya 20” kwa juhudi zake za kuendeleza Teknolojia ya Habari na
Mawasiliano (TEHAMA).
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :