SERIKALI YA MAPIDUZI ZANZIBAR KUPAMBANA NA WAUZA DAWA ZA KULEVYA
Posted in
No comments
Wednesday, June 27, 2012
By
danielmjema.blogspot.com
SERIKALI
ya Mapinduzi Zanzibar imesema imedhamiria kwa dhati kupambana na madawa ya
kulevya nchini na kuwaomba wananchi wasaidie juhudi hizo.
Hayo
yameelezwa jana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar,
Fatma Abdul-habib Ferej alipokuwa akijibu msuali ya wajumbe wa baraza la
wawakilishi huko Chukwani Mjini Zanzibar.
Awali
katika suali la msingi la Mwakilishi wa nafasi za wanawake (CCM) Panya Ali
Abdallah alisema miaka sita tangu washirika wa maendeleo UNDP kutoa msaada wa
choo cha flashi cha madawa ya kulevya ambacho kilitegemewa kufungwa katika
uwanja wa ndege na kuhoji ni sababu zipi zilizopelekea choo hicho kutofungwa
hadi sasa.
Akijibu
suali hilo Waziri Fatma alisema alisema sababu za kuchelewa kufungwa choo hicho
ni pamoja na kutopatiwa kwa eneo muwafaka mapema kwa mamlaka husika kwa ajili ya
kujenga choo hicho hasa kwa kuzingatia mazingira ya eneo husika.
Aliwaambia
wajumbe wa baraza la wawakilishi kwamba msukumo mkubwa wa hatua iliyofikiwa sasa
ilichangiwa kwa kiasi kikubwa na mwenyekiti wa tume kwa wakati huo.
“Napenda
kumjulisha mheshimiwa mjumbe kwamba choo hicho sasa kiemshafungwa, yaliobaki ni
mambo madogo madogo tu ya kumalizia ili kianze kutumika” alisema Waziri
huyo.
Akijibu
suali la mwakilishi huyo kwamba haoni kama kuchelewa kutoa huduma kwa choo hicho
kutaweza kuwavunja moyo washirika wa maendeleo, kitendo hicho cha kuchelewa
kinaweza kutafsiriwa hivyo.
“Napenda
kuungana na mjumbe katika hilo kuwa kitendo chetu cha kuchelewa kinaweza
kutafsiriwa na washirika wa maendeoe kuwa ni kuwavunja moyo katika mapambano
dhdii ya ya madawa ya kulevya” alisema.
Hata
hivyo alisema nia na lengo la serikali kwa ujumla katika vita dhdii ya dawa za
kulevya ni thabiti na ila lengo la kuona kwamba inatumia zahudi zake zote katika
kukabiliana na janga la madawa ya kulevya.
Waziri
Fatma alisema usalama wa uwanja wa ndege ni muhimu kwa wageni na weneywe na
serikali inaendelea na juhudi za kupambana na waletaji na wasafirishaji wa
madawa hayo.
Akijibu
suala la kukosekana kwa choo hicho kunazorotesha juhudi za mapambano dhidi ya
madawa ya kulevya, Waziri alisema kutokuwepo kwa choo katika uwanja bado
hakujaathiri shughuli za kupambana na madawa ya kulevya.
“Kwa
kweli naomba niseme kwamba kukosekana kwa choo hakujaathiri hata kidogo vita
dhidi ya madawa ya kulevya kwa sababu wanaohusika wanawachukua watuhumiwa na
kuwapeleka katika hospitali ya mnazi mmoja na kazi hizo hufanywa huko”alisema
Waziri huyo.
Aidha
alitoa wito kwa taasisi za dola zilizopewa majukumu ya udhibiti kuunga mkono
juhudi za serikali na washirika wa maendeleo katika kukabiliana na janga
hilo.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :