Nani Atakutana Na Spain Kwenye Fainali?- Olle Anajibu!

Posted in
No comments
Thursday, June 28, 2012 By danielmjema.blogspot.com



Ni swali jepesi, ni Ujerumani! Ujerumani ndio nchi pekee hadi sasa ambayo haijapoteza hata mechi moja. Na ndio timu iliyofunga mabao mengi kwenye EURO inayoendelea sasa. Naamini Ujerumani ndio timu iliyokuja na kikosi kizuri kwenye fainali hizi. Na wana wachezaji mahiri karibu katika kila Idara. Wanacheza mpira wa mashambulizi kama ule wa Hispania. Na wanacheza kwa kupiga pasi nyingi.
 

Italia nao wana timu nzuri katika mashindano haya wakiwa na wachezaji wengi vijana. Ni kama vile Balotelli. Italia nao ni wazuri kwa kucheza soka ya mashambulizi, lakini pia wana ngome imara inayoongozwa na De Rossi. Muhimu kwa Italia leo ni ngome yao, kwa vile watacheza na timu yenye kushambulia sana. Italia ina wachezaji wachache wenye kasi, lakini si wengi. Hivyo itakuwa vigumu kwa Italia kufanya counter attack dhidi ya Ujerumani. Hivyo, natabiri mechi ya leo itamalizika na matokeo ya 2-1 kwa Ujerumani. Tusubiri tuone!

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .