Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari...!
Posted in
No comments
Friday, August 24, 2012
By
danielmjema.blogspot.com
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
24 AGOSTI 2012
MABADILIKO YA RATIBA YA UCHAGUZI WA VYAMA WANACHAMA WA TFF
Kamati
ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imefanya
mabadiliko madogo katika ratiba za uchaguzi za wanachama wa TFF. Ratiba
za uchaguzi za vyama wanachama wa TFF ambavyo vimekwishaanza mchakato na
ambavyo havijaanza mchakato wa uchaguzi itakuwa kama ifuatavyo:
CHAMA MWANACHAMA WA TFFTarehe ya Kuanza Mchakato wa uchaguziTarehe ya Uchaguzi
Arusha Region Football Association (ARFA)27-Aug-20127-Oct-2012
Dar es Salaam Region Football Association (DRFA)3-Sep-201214-Oct-2012
Geita Region Football Association (GEREFA)29-Sep-201210-Nov-2012
Iringa Region Football Association (IRFA)28-Jul-20128-Sep-2012
Katavi Region Football Association 29-Sep-201210-Nov-2012
Kigoma Region Football Association (KRFA)21-Jul-20121-Sep-2012
Kilimanjaro Region Football Association (KRFA)31-Jul-20128-Sep-2012
Lindi Region Football Association (LIREFA)8-Sep-201220-Oct-2012
Manyara Region Football Association (MARFA)21-Jul-201215-Sep-2012
Mbeya Region Football Association (MREFA)8-Sep-201221-Oct-2012
Mwanza Region Football Association (MZFA)29-Sep-20128-Nov-2012
Njombe Region Football Association (NJOREFA)4-Aug-201215-Sep-2012
Coast Region Football Association (COREFA)3-Sep-201214-Oct-2012
Rukwa Region Football Association (RUREFA)27-Aug-20127-Oct-2012
Football Association of Ruvuma (FARU)22-Sep-20123-Nov-2012
Shinyanga Region Football Association (SHIREFA)8-Sep-201220-Oct-2012
Simiyu Region Football Association (SIFA)15-Sep-201227-Oct-2012
Tabora Region Football Association (TAREFA)27-Aug-20126-Oct-2012
Tanga Region Football Association (TREFA)22-Sep-20123-Nov-2012
Tanzania Football Coaches Association (TAFCA)29-Sep-201210-Nov-2012
Tanzania Sports Medicine Association (TASMA)15-Sep-201227-Oct-2012
Soccer Players Union of Tanzania ( SPUTANZA)15-Sep-201228-Oct-2012
Football Referee’s Association of Tanzania (FRAT)21-Aug-201230-Sep-2012
Tanzania Women Football Association (TWFA)22-Sep-20124-Nov-2012
TFF
inavitaka vyama wanachama wake kuzingatia kikamilifu ratiba hii
iliyotolewa na Kamati ya Uchaguzi ya TFF na Kanuni za uchaguzi za
wanachama wa TFF katika kutimiza wajibu wao wa kikatiba.
Kamati
ya Uchaguzi ya TFF haitabadilisha ratiba hiyo kutokana na wilaya yoyote
kutokamilisha uchaguzi wake, na hivyo inazitaka Kamati za Uchaguzi za
Mikoa kuhakikisha chaguzi zinafanyika kwa mujibu wa ratiba hii.
Kamati
pia inazitaka Kamati za Uchaguzi za Mikoa kusimamia kikamilifu na kwa
umakini chaguzi za wilaya zinazoendelea kwenye wilaya zilizo mikoani
kwao. Ni muhimu kwa kamati kuhakikisha Kanuni za Uchaguzi za Wanachama
wa TFF zinafuatwa na kusimamiwa kwa umakini.
Kamati
ya Uchaguzi ya TFF pia imebaini kuwa kuna Kamati za Uchaguzi za Mikoa
ambazo hazikusimamia kikamilifu chaguzi za viongozi wa wilaya, kitu
ambacho kinaweza kusababisha matatizo hapo baadaye. Kwa mara nyingine,
Kamati ya Uchaguzi ya TFF inazitaka Kamati za Uchaguzi za Mikoa
kuhakikisha wanaoomba kugombea uongozi kwenye wilaya, wana sifa
zinazolingana na utashi wa Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF na
Katiba.
Wanachama
ambao hawakuzingatia ratiba hiyo, hawatapewa fursa nyingine ya
kubadilisha tarehe za uchaguzi na hilo litakapotokea hatua za kikanuni
zitachukuliwa.
Angetile Osiah
KATIBU MKUU
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :