UZNDUZI WA SERENGETI FIESTA 2012-MJINI MOSHI NI BHAAAAAS ARIFU!
Posted in
No comments
Saturday, August 25, 2012
By
danielmjema.blogspot.com

Wasanii
machachari Bongo Move Wema Sepetu (kushoto) na Aunt Ezekiel wakicheza
muziki wa bongo Fleva uliokuwa ukishushwa na Msanii wa Bongofleva,Ferooz
katika uzinduzi wa Tamasha la Serengeti Fiesta 2012 Bhaaaaass! katika
Uwanja wa Chuo cha Ushirika Mjini Moshi usiku huu. Tamasha hilo
limebamba ile mbaya.
Mkuu
wa mkoa wa Kilimanjaro,Mh Leonidas Gama akimtaja mshindi
aliyejinyakulia gari aina ya Vits iliyokuwa ikinadiwa kwenye tamasha la
Serengeti Fiesta 2012,maara baada ya kuchezeshwa droo usiku huu,pichani
mwanzo kulia ni Mkurugenzi wa Masoko kampuni ya bia ya Serengeti,Ephraim
Mafuru,Muwakilishi kutoka michezo ya bahati nasibu ya Taifa,Abdallah
Mohamed akishuhudia tukio hilo,na mwisho kushoto ni Mkurugenzi wa
kampuni ya Clouds Media Group,Joseph Kusaga pamoja na Mkuu wa Wilaya ya
Moshi Mjini,Mh Dr Msengi wakishuhudia tukio hilo usiku huu ndani ya
uwanja wa chuo cha ushirika.
Mkuu
wa mkoa wa Kilimanjaro,Mh Leonidas Gama sambamba na Mkuu wa Wilaya ya
Moshi Mjini,Mh Dr Msengia wakiingia kwa shangwe kwenye jukwaa la
Serengeti Fiesta 2012 usiku huu kwa ajili ya kulizindua tamasha hilo
ambalo limepokelewa vyema kwa wakazi wa mji huo na vitongoji
vyake.Pichani kulia ni Dj Zero akikamua vilivyo.
Dj
Pq kutoka Clouds FM akikamua vilivyo kwenye mashine,kati ni mtangazaji
wa Clouds FM B Dozen na mdau mwingine wakifuatilia kwa makini makamuzi
yanayoendelea usiku huu,ambapo washabiki kibao wamejitokeza ndani ya
uwanja wa chuo cha ushirika.
Pichani
shoto ni msanii kutoka THT,Recho sambamba na wacheza shoo wake
wakitumbuiza jukwaani usiku huu ndani ya tamasha la Serengeti Fiesta
2012.
Moja ya kikundi mahiri kutoka THT kkikionesha mbwembwe zake jukwaani.
Dj Zero akikamua vilivyo.
Moja ya kikundi cha THT kikiwa katika picha ya pamoja.
Baadhi
ya wakazi wa mji wa Moshi na vitongoji vyake waliojitokeza kwenye
tamasha la Serengeti Fiesta usiku huu ndani ya Uwanja wa chuo cha
Ushirika mjini Moshi.
Baadhi ya wasanii nyota wa filamu nchini nao wakishuhudia tamasha la Serengeti Fiesta usiku huu.
Hapatoshi usiku huu.
Msanii wa kizazi kipya Sheta akiwaimbisha washabiki wake waliojitokeza kwa wingi usiku huu ndani ya tamasha la Serengeti.

Ferooz akiwa na mmoja wa mashabiki wake wakilishambulia jukwaa vilivyo.

Sehemu
ya wakazi wa mji wa Moshi wakiendelea kushuhudia makamuzi ya wasanii
mbalimbali wanaotumbuiza usiku huu kwenye uzinduzi wa tamasha la
Serengeti Fiesta 2012.

Prezoo
akiwarusha mashabiki kibao (hawapo pichani) waliojitokeza jioni ya leo
kwenye uzinduzi wa tamasha la Serengeti Fiesta 2012
Pichani
juu na chini ni mwanamuziki kutoka nchini Kenya na mmoja wa shiriki wa
shindano la Big Brother Stargame,CMB Prezoo akitumbuiza jukwaani usiku
huu kwenye uzinduzi wa tamasha la Serengeti Fiesta 2012 ndani ya uwanja
wa chuo cha ushirika mjini Moshi.
Mmoja
wa wasanii wa hip hop Joh Makini akikamua vilivyo usiku huu mbele ya
umati mkubwa wa watu uliojitokeza kwenye uzinduzi wa tamasha la Fiesta.
Msanii mahiri wa bongofleva,Lina akiwa na densaz wake wakilishambulia jukwaa vilivyo.
Lina akiimba wimbo wake Yalaiti
Mkali mwingine wa hip hop Mwana FA akishusha mitindo huru.
Pichani
juu na chini Mwana FA akilishambulia jukwaa vilivyo kwa mitindo yake
huru iliyokuna vilivyo mashabiki wake,waliofika kwa wingi kwenye tamasha
la Serengeti Fiesta 2012.
Wasanii
wa nyota wa Filamu hapa nchini nao walijumuika kwa pamoja kwenye
uzinduzi wa tamasha la Serengeti Fiesta 2012,pichani jukwaani ni Wema
Sepetu,Jacob Steven a.k.a JB,pamoja na Aunt Ezekiel wakilisakata sebene.
Ray nae akilisakata sebene vilivyo.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :