MUIGIZAJI JOHN STEPHANO ALIYEFARIKI DUNIA JUZI, KUZIKWA JUMANNE MAKABURI YA KINONDONIO MOVIE....R.I.P JOHN MAGANGA

Posted in
No comments
Saturday, November 24, 2012 By danielmjema.blogspot.com

"REST IN PEACE BRO,kwa wale tuliopiga Green kwa Bujugo mtakuwa mnamkumbuka this guy,dah,he passed away jana,what a loss"-geoffrey Lea

REST IN PEASE JOHN STEPHANO MAGANGA

  JOHN MAGANGA enzi za uhai wake.
TASNIA ya filamu nchini Tanzania, imefikwa na msiba mwingine Mkubwa wa Msanii wa Filamu, John Stephano Maganga aliyefariki jana katika Hospitali ya Muhimbili baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa viongozi wa Wasanii zinasema kuwa Mipango ya mazishi inafanyika Nyumbani kwao Mwananyama A jirani na Kopakabana Bar  jijini Dar es Salaam.

Marehemu John anaetarajiwa kuzikwa siku ya jumanne Makaburi ya Kinondoni Dar es Salaam, alianza kujiingiza katika sanaa ya uigizaji mwaka 2001 chini Thea na Deo Shija na ilipofika mwaka 2008 alianza kuigiza filamu na hadi mauti yanamfika alikuwa njiani kutoa Filamu yake.

Aidha Wasanii wote wanataarifiwa kufika katika Kikao Maalum Nyumbani kwa John Stephan oleo Saa tisa alasiri kwaajili ya kupanga mikakati, ya mazishi.

Pia Mtanzania yeyote atakae guswa na Msiba huu anaweza kutuma Rambi Rambi zake kupitia Namba ya Tigo Pesa za 0715541714 au 0718951355

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .