UZINDUZI WA KILIMANJARO MARATHON 2013 KATIKA UKUMBI WA MORIO MOSHI
Posted in
No comments
Saturday, December 1, 2012
By
danielmjema.blogspot.com
IBRAHIMU MSENGI-DC MOSHI |
INSP.LISTON NEPACHA MWENYEKITI KAA |
ALLEN MARO-TPC |
GEORGE KAVISHE- MENEJA KILIMANJARO PREMIUM LAGER |
MSIMU wa kumi na moja wa mbio za kimataifa za Kilimanjaro Marathon
zinazotarajiwa kufanyika Machi 3, mwaka 2013, umezinduliwa Rasmi hapo Jana
Mjini hapa katika Ukumbi wa Morio Hall.
Akizungumza katika uzinduzi huo Meneja wa Bia ya Kilimanjaro
Premium Lager ambayo ndiyo wamekuwa wadhamini wakuu wa mbio hizo tangu
zilipoanzishwa mwaka 2003, George Kavishe alisema, wao kama wadhamini wakuu
wamedhamiria kufanya mabadiliko makubwa katika mbio hizo na kuzifanya kuwa na
hadhi ya kimataifa zaidi.
“Sisi kama wadhamini wakuu wa mbio hizi zinazoshirikisha
wakimbiaji kutoka kila kona ya Dunia, tumedhamiria kuhakikisha tunaboresha mbio
hizi na kuzifanya kuwa sura ya kimataifa,” alisema Kavishe
Alisema kutokana na matokeo ya mbio za mwaka huu,
yaliyofanyika mapema Februari, na kushuhudia
wakenya wakitawala mbio hizo, safari
hii wamejipanga kwa kutoa changamoto ya zawadi zaidi ya kawaida kwa mshindi wa
kwanza kutoka Tanzania ambapo kwa mshindi wa kwanza, wanaume na wanawake kutoka
Tanzania atapata Shilingi milioni sita ikiwa ni mara mbili zaidi ya zawadi za
kawaida.
“Tumeboresha mashindano nah ii ni kitu kipya , kwani kutokan
ana aibu ya mashindano ya mwaka huu, mwaka ujao kila mshindi wa kwanza kutoka
ndani ya nchi atapata maara mbili ya fedha za mshindi wa kwanza,” alisema
Kavishe.
Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama
katika hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na Mkuu wa wilaya ya Moshi,
Dkt.Ibrahimu Msengi, aliwataka wanariadha wote watakaoshiriki kuhakikisha kuwa
kile kilichotokea katika mashindano ya liyopita hasa ya mwaka huu yanbaki kuwa
sehemu ya Historia.
Alisema Mkoa umefurahishwa sana kuwepo kwa mashindano hayo
mkoani hapa na antarajia mbio hizo zitachangia katika kukuza sekta ya Utalii,
Uchumi na mahusiano ya kimataifa kutokana na kushirikisha wakimbiaji kutoka
mataifa mbalimbali kutoka katika kila kona ya dunia.
Wakati huohuo Mwenyekiti wa chama cha Riadha mkoani
Kilimanjaro (KAA), Liston Nepacha alibainisha kuwa kwa kushirikiana na chama cha
Riadha Taifa (RT), wamedhamiria kufuta mapungufu yote yaliyojitokeza katika
mbio za mwaka huu na kuongeza kuwa tayari ya kikosi cha Tanzania kinaendelea na
Maandalizi katika Kambi yaop iliyoko Holili, Himo mkoani Hapa.
Mashindano ya Kilimanjaro Marathon yanayofanyika kila Mwaka
yanadhaminiwa na Kilimanjaro premium Lager, Kilimanjaro Drinking Water, Arusha
Hotel, Gapco wanaodhamini mbio za watu wenye Ulemavu, Bonite, Kiss Hotel, TPC,
Shoprite, KK security, Simba Cement, Merenga Investment, CFAO Motors na
yanatarajia kuwa na washiriki wapatao 6000.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :