

Huu ni mchezo ambao takwimu zilikuwa zinaibeba Real Madrid kwa kiasi kikubwa kulikoMan City ambao walikuwa nyumbani, 24 July 2015 Man City akiwa nyumbani alifungwa goli 4-1 na 21 Nov 2012 alitoa sare ya goli 1-1 katika uwanja huo wa Etihad, takwimu ambazo hazioneshi dalili nzuri akicheza na Real Madrid katika uwanja huo.

Licha ya kuwa mchezo umemalizika kwa sare ya 0-0, Real Madrid kwa mujibu wa takwimu walikuwa wanatajwa kuwa na safu imara ya ushambuliaji kuliko Man City , kwaniReal katika mechi zake tano zilizopita hivi karibuni walikuwa wamefunga jumla ya magoli 18 na kufungwa matatu, wakati Man City walikuwa wamefunga magoli 11 na kufungwa mawili.
No comments:
Post a Comment