Askofu Mokiwa Acharuka
Posted in
No comments
Thursday, May 31, 2012
By
danielmjema.blogspot.com
RAIS
wa Umoja wa Maaskofu Afrika Mashariki na Kiongozi wa Kanisa la
Anglikana Tanzania, Askofu Dk Valentino Mokiwa amesema waumini Wakristo
hawaridhishwi na utendaji kazi wa Polisi ukiwemo ufuatiliaji wa matukio
ya kuchomwa moto kwa makanisa visiwani Zanzibar.
Akizungumza
katika kikao kilichokutanisha viongozi wa Dini na Serikali katika Ofisi
ya Makamu wa Pili wa Rais jana, Dk Mokiwa alisema Polisi imeshindwa
kufuatilia matukio ya uhalifu ikiwa ni pamoja na kuchomwa kwa makanisa
hayo.
Alisema tangu mwaka jana zaidi ya makanisa 25 yamechomwa moto na hakuna kesi iliyofikishwa mahakamani.
“Matukio
mengi ya kuchomwa moto kwa makanisa yamejitokeza Zanzibar tangu mwaka
jana lakini hakuna kesi iliyofikishwa mahakamani au mtu aliyekamatwa,”
alisema Dk Mokiwa.
Aidha,
alisema hadi sasa wafuasi Wakristo wanafanya kazi zao kwa hofu na
wasiwasi kwani baadhi ya watu bado wanashambulia nyumba za ibada ikiwa
ni pamoja na kurusha mawe.
“Hadi
sasa wafuasi wetu wanafanya kazi zao kwa wasiwasi mkubwa hata katika
nyumba za ibada kwani wafuasi wenye siasa kali wanarusha mawe katika
nyumba za ibada,” alisema.
Dk
Mokiwa alisema hakubaliani na kauli za baadhi ya watu kwamba wanaofanya
vitendo hivyo ni wahuni, bila hatua za kisheria kuchukuliwa dhidi yao.
Alifafanua,
kuwa kama ni suala la Muungano kwa nini watu hao wachome moto makanisa
na wasisubiri Tume ya Kuratibu Maoni ya Katiba ili wawasilishe hoja zao
kuhusu Muungano.
“Sisi
hadi sasa hatuamini kwamba wanaofanya fujo ni wahuni, kama ni wahuni
kwa nini wanachoma moto makanisa na kama ni Muungano kwa nini wasisubiri
Tume ya Katiba? “Alihoji Askofu Mokiwa.
Mapema
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohamed Aboud akijibu
baadhi ya hoja za Baraza la Maaskofu Tanzania, alisema tayari Serikali
imeweka ulinzi wa kutosha kwa makanisa yote visiwani hapa.
“Tumeweka
ulinzi katika sehemu zote za nyumba za ibada ikiwamo makanisani na
Serikali itahakikisha hakuna fujo zitakazojitokeza kwa sasa,” alisema
Aboud.
Aliahidi
kuwasilisha kwa Rais Dk Ali Mohamed Shein malalamiko yao yote kuhusu
vitendo vya kuwadhalilisha Wakristo visiwani huku Tanzania ikiwa nchi
isiyo na dini isipokuwa wananchi.
Mapema
viongozi hao walitaka kuonana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi (SMZ) kuzungumzia matukio hayo yenye kuashiria
uvunjifu wa amani na utulivu.
Hata
hivyo Aboud alikiri akisema wapo watu wanatumia vibaya taasisi za
kidini kama mwamvuli wa kisiasa katika kuwasilisha hoja zao mbalimbali,
yakiwamo masuala ya Muungano na marekebisho ya Katiba
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :