Benki Ya Wakulima Kuanza
Posted in
No comments
Thursday, May 31, 2012
By
danielmjema.blogspot.com
SERIKALI
imesema kuwa Benki ya Wakulima inatarajiwa kukamilika wakati wowote
mwaka huu na kuanza kutoa mikopo mikubwa na ya muda mrefu ili kuboresha
sekta ya kilimo nchini iliyo tegemeo kubwa katika kutoa ajira na
kuongeza kipato cha wananchi wengi.
Aidha,
serikali pia imekubali kuongeza mtaji kwenye Benki ya Rasilimali nchini
(TIB) ili kuiwezesha kuwa na uwezo wa kutoa fedha zitakazotumika kwenye
miradi mbalimbali ya maendeleo hapa nchini, ikiwemo ya uboreshaji wa
miundombinu.
Hayo
yalisemwa jana na Naibu Waziri wa Fedha, Janeth Mbene mara baada ya
kufungua mkutano mkuu wa 38 wa Taasisi za Benki za Maendeleo barani
Afrika (AADFI) unaofanyika jijini hapa chini ya uenyekiti wa Mkurugenzi
Mtendaji wa TIB, Peter Noni.
Mbene
alisema kuwa, serikali imekubali kutenga kati ya dola za Marekani
milioni 400 na 500 kwa ajili hiyo ambapo benki hiyo ya wakulima
inatarajiwa...Somba zaidi http://www.freemedia.co.tz
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :