WAZIRI MATHAYO KUFUNGA MAADHIMISHO YA MAZIWA MKOANI KILIMANJARO
Posted in
No comments
Thursday, May 31, 2012
By
danielmjema.blogspot.com
WAZIRI wa kilimo na mifugo
David Mathayo David anatarajiwa
kufika kesho mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya kufunga maadhimisho ya wiki ya
maziwa ambayo kitaifa kwa mwaka huu yamefanyika mkoani Kilimanjaro.
Maadhimisho hayo yalianza tarehe 29 mei na kilele chake kinatarijiwa kuhitimishwa rasmi
tarehe 01 juni mwaka huu, ambapo pamoja na waziri kufunga maonesho hayo pia
atapata fursa ya kutembelea mabanda mbalimbali
ya bidhaa za maziwa yaliyopo kwenye viwanja vya mashujaa vilivyopo katika
manispaa ya moshi, mkoani kilimanjaro na kukutana na wadau mbalimbali wa sekta
ya kilimo na ufugaji mkoani Kilimanjaro.
Aidha wakiongea kwa nyakati
na KIJIWE, baadhi ya wadau wa maziwa walilalamikia mwamko
mdogo miongoni mwa wananchi kuhusu umuhimu wa maziwa na kutupia lawama kwa
viongozi wa idara ya kilimo na mifugo mkoani Kilimanjaro kwa kushindwa kutoa
elimu ya kutosha kwa wananchi.
Mmoja wa wadau hao Maxi mwenda , ambaye ni msindakaji kutoka
Mountain Drinking cha Usariver mkoani Arusha, alisema Kilimanjaro inazalisha
maziwa kwa wingi sana lakini cha kushangaza ni kitendo cha wananchi
kutojitokeza katika maenesho hayo na lawama zote akizielekeza kwa bodi ya
maziwa Tanzania pamoja na uongozi wa kilimo mkoani hapo.
“Katika mikoa yote Kilimanjaro, inaongoza kwa uzalishaji wa maziwa lakini cha kushangaza kama unavyoona,
wananchi hawajajitokeza kwa wingi kama tulivyotarajia katika maenesho haya, sasa kwa mtazamo huo
inaonesha kwamba wananchi hawatumii kabisa bidhaa hii au mwamko na elimu kuhusu
umuhimu wa maziwa ni mdogo, nadhani ni vyema bodi na uongozi katika maandalizi
yao ya maenesho yajayo waliangalie hilo,” alisema Mwenda.
Kwa upandewao wananchi,
walionyesha kushtushwa na taarifa za maadhimisho hayo kuandaliwa mkoani
hapo na kuelekeza lawama zao kwa uongozi wa mkoa kwa kutowapa taarifa hali
iliyopelekea maenesho hayo kupooza na kudai kwamba huo ni uzembe mkubwa
unaokwamisha shughuli za Maendeleo mkoani kilimanjaro.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :