Monday, June 18, 2012

Athari Gani Wanandoa Wanapotengana Wakiwa Na Watoto?





Wawili hawa wanapendana.wa kulia alikuwa mke wa kwanza ila bahati mbaya wakaachana na bwana akamuoa bibi wa kushoto.wote wamepata watoto,lakini watoto wanaishi na baba yao kwa hiyo na mke wa sasa.Yule ambaye waliachana huja kuwatembelea watoto wake.jana nilikutana nao kwa pamoja na kuna baadhi ya mambo yalijitokeza

1.Mke wa zamani alikuwa akilia kwani amewamiss wanaye na watoto walikuwa wakilia muda wote wakiwa na mama yao
2.Ilibidi mke wa zamani amwombe mke wa sasa amwombee ruhusa kwa mume wake wa zamani ili aende na mtoto wake atamrudisha baada ya siku chache.Licha ya mke wa sasa kukubali,mume wake alikataa kumruhusu mtoto kuondoka na mama yake,kitu kilichoongeza majonzi kwa mtoto na mama yake
3.wakati wa kuondoka mke wa sasa na mume wa zamani kwa pamoja walimsindikiza,na baadaye alilalamika kwangu kuwa hakupata privacy ya kujadili hali ya watoto wake na mume wake wa zamani.
Kwa kweli kuachana kuna athari kubwa sana.Niliwaeleza kutumia habari yao kwenye mtandao wakaniruhusu

No comments:

Post a Comment