CLOUDSFM, PRIMETIME PROMOTIONS WAZINDUA FIESTA 2012
Posted in
No comments
Friday, June 29, 2012
By
danielmjema.blogspot.com
Serengeti
Fiesta ni Msimu Maalum kwa ajili ya wapenzi na wadau wote wa muziki,
Utamaduni na Burudani ambapo kwa karibu miezi miwili Watanzania kwenye
Mikoa zaidi ya 12 nchini Tanzania wataweza kuendeleza msimu wa Dhahabu
kwa kushuhudia jukwaa lenye uweledi na mvuto kutokana na Burudani
hadhara ya wasanii mbalimbali wanaochipukia na wenye majina na umaarufu
mkubwa..FIESTA 2012..BHAAAAAAS!!!
kampeni meneja wa Push Mobile Mr,Rugabo akiwa na Barbra Hasan akionyesha jinsi ya kushiriki na ushinde haya magari na pikipiki
Mkuu wa vipindi radio Clouds akitoa maelekezo juu ya Fiesta 2012
KAULI
MBIU FIESTA 2012- Ni "Ni Muonekano Mpya - Burudani Ile
Ile..Bhaaaaas!!!" Hii Inatokana na kwamba Serengeti Fiesta imeweza kuwa
sehemu muhimu ya Burudani katika Maisha ya Vijana wa Kitanzania kwa
miaka 10 ya uhai wake. Hivyo mwaka wa 11
kamati Kuu ya maandalizi ya Serengeti Fiesta imedhamiria kuongeza
ufanisi wake kwa kuhusisha mambo mapya yenye kuleta tija kwa wapenzi na
wafuatiliaji wa Serengeti Fiesta 2012 kwa kuzingatia kiwango kile kile
cha Burudani kinachozalishwa na Serengeti Fiesta, Neno Bhaaaaaaaas!!!
linasisitiza dhamira hii ya Tamasha husika..Fiesta 2012..Bhaaaaaaaaa!!!
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :