GIDABUDAY KUONGOZA MSAFARA YA WAKONGWE KILI MARATHON
Posted in
No comments
Thursday, February 28, 2013
By
danielmjema.blogspot.com
Mwanariadha hapa nchini na
mwanaharakati wa mageuzi katika michezo, Wilhelm Gidabuday amethibitisha
kuongoza timu ya wakongwe wenzake katika mbio za mwaka huu za Kiliamnjaro
Marathon yanayotarajia kufanyika jumapili ya Machi 3 mjini hapa.
Gidabuday amesema wameamua
kuja Kilimanjaro Marathon mwaka 2013 kwa lengo moja tu, kuwaunga mkono
wakimbiaji wa kitanzania na kuhakikisha kuwa mbio za mwaka hazirudii makosa ya
miaka ya nyuma.
Amesema kuwa mbio za Kilimanjaro
marathon ni mbio kubwa kuliko zote Tanzania na hivyo ni vizuri watanzania
wakijionea ufahari wa kuandaa mbio kubwa kama hizi katika ardhi yao huku akiwashukuru
waandaaji wa mbio hizi kwa jitihada zao kufanya mbio hizi kuwa za kimataifa
zaidi.
Amewataja wanariadha wakongwe atakaoongozana nao, wakiwemo
wanaokimbia hadi hivi sasa, kuwa ni pamoja na Andrea Sambu ambaye aliwahi kuwa
bingwa wa dunia pekee Mtanzania katika mbio za nyika za dunia mwaka 1991,
Faustin Baha Sule, ambaye ni mshindi wa medali ya fedha mbio za nusu marathon
2000.
Wengine ni Rogath John
Akhwari aliyeiwakilisha nchi katika mbio kadhaa za nyika za dunia, Getuli Bayo, Michael Sarwatt, Thadeo
Nada na Anthony Mwingereza ambao kwa pamoja wamewahi kupeperusha vyema bendera
la Taifa.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :