WANAWAKE 10 WAPANDA MLIMA KILIMANJARO KUHAMASISHA USWA WA KIJINSIA
Posted in
No comments
Thursday, February 28, 2013
By
danielmjema.blogspot.com
Wakiwa wamewahi kufanikiwa kupanda mlima mrefu zaidi
duniani, mlima wa Evarest, wanawake saba katika nchi ya Nepal wanaungana na
wenzao watatu kutoka afrika akiwemo msanii maarufu wa Tamthilia ya Isidingo,
Hlubi Mboya maarufu kwa jina la Nandipha.
Akizungumza katika hafla ya kuwaaga wapandaji hao,
Mkurugenzi wa shirika la chakula duniani nchini Tanzania (WFP), Richard Ragan
amesema kuwa la la elimu, kutokana na mamba za mapema, kuolewa wakiwa wadogo
pamoja na changamoto ya kukosa fedha za kumudu mahitaji yao na ndio maana
wameamua kuwaunganisha katika kueneza elimu ya usawa na ukombozi wa mwanamke.
Ragan amefafanua kuwa mmoja wa wapandaji kutoka Nepali aliwahi kutoroka nyumbani akiwa na umri wa miaka 14, kukimbia unyanyasaji aliokuwa akifanyiwa na ndugu zake pamoja na shinikizo za kuolewa.
Katika msafara huo wapo Watanzania Wawili, Ashura
Kayupayupa, ambaye ni mwanaharakati dhidi ya ndoa za mapema na Mwalimu Anna
Philipo ambaye ni Mwanaharakati dhidi ya unyanyasaji wa kijinsia kutoka katika
jamii ya Wahadzabe.
Kutoka Nepal ni Shailee Basnet, Pujan Acharya, Nimdoma
Sherpa, Pema Diki Sherpa, Chunu Shretha, Asha Kumari Singh na Maya Gurang,
pamoja na wapiga picha wawili James Gimbrone na Russ Paraseau.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :