WFP IMEWATAKA WATANZIA KUTUMIA VIZURI CHAKULA KUEPUKA KUKABILIWA NA NJAA
Posted in
No comments
Thursday, February 28, 2013
By
danielmjema.blogspot.com
NANDIPHA |
Shirika la chakula duniani (WFP), limewataka
watanzania kuhakikisha wanajiwekea utaratibu mzuri wa matumizi ya chakula ili
kuepuka kukumbwa na baa la njaa.
Balozi wa WFP afrika dhidi ya njaa, Hlubi Mboya,
maarufu Nandipha, ambaye yuko nchini Tanzania ameyasema hayo leo muda mfupi
kabla ya kuongoza timu ya wanawake wapatao kumi kupanda mlima Kilimanjaro
kuhamasisha usawa wa kijinsia.
Akizungumza na wandishi wa habari, Nandipha amesema
kuwa kwa sasa hali ya chakula duniani inasikitisha na kutisha sana hivyo ni
bora watu hasa watanzania wakawa makini na matumizi ya chakula ili kuepuka
kujiingiza katika matatizo na ukosefu wa chakula.
Amesema kuwa watu wengi wamekuwa na tabia ya kufuja
chakula pindi wanapopata mavuno ya ziada na kusahau kuwa kuna mahali ambapo
watu wanakufa njaa kila sekunde kwa hitaji la chakula.
Amesema WFP imekuwa ikifanya kazi na shule mbalimbali
kuhakikisha watoto wadogoambao ndio wahanga wakubwa wa njaa, wanapata chakula
cha kutosha huku akiishukuru serikali ya Tanzania kupitia kwa shirika la mpango
wa kupunguza njaa na kuhamasisha maendeleo Tanzania (UNDAP 2011-2015).
RAGAN WA WFP AKIWA NA CHARLES KUTOKA CHILDREACH KATIKA GETI LA MACHAME LEO |
Nandipha amesema kwa sasa anazunguka dunia nzima na
hasa Afrika, kuhamasisha sera ya chakula mashuleni, chakula kama rasilimali na
kuongeza kwamba tayari ameshatembea kwenye nchi za Sudan, Ghana na Congo pamoja
na Aerika Kusini anakotokea.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa shirika la chakula
WFP nchini Tanzania, Richard Ragan amesema kuwa, mpango wa WFP katika bara la
Afrika ni kutokomeza njaa na sio vinginevyo huku akisisitiza umuhimu wa
kuhifadhi na kutunza chakula.
zoezi hilo limeandaliwa na shirika lisiso la kiserakali la kuhudumia watoto la Childreach Tanzania, Shirikala chakula duniani, WFP, hifadhi ya taifa TANZANIA, kwa ushirikiano na
zoezi hilo limeandaliwa na shirika lisiso la kiserakali la kuhudumia watoto la Childreach Tanzania, Shirikala chakula duniani, WFP, hifadhi ya taifa TANZANIA, kwa ushirikiano na
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :