NANDIPHA WA ISIDINGO ATAMANI KUFANYA KAZI NA BONGO MOVIE
Posted in
No comments
Wednesday, February 27, 2013
By
danielmjema.blogspot.com
MSANII wa Tamthilia ya Isidingo, Hlubi Mboya,
Maarufu kama Nantipa, kutoka afrika kusini amekiri kuwa moja ya ndoto zake ni kufanya
kazi na wasanii wa filamu wa hapa nchini.
Msanii huyo ambaye ni balozi wa shirika la Chakula
duniani WFP, anatarajiwa kuongoza timu ya Wanawake 12 kutoka katika nchi za Tanzania, Nepal na Australia kupanda
mlima Kilimanjaro kesho kupitia Geti la Machame lililok wilaya ya Hai, Mkoani
hapa.
Alisema wasanii wengi baada ya kupata umaarufu
hujisahau na kujikuta wakijiingiza katika matumizi mabaya ya madawa ya kulevya
pamoja na kufanya vitendo viovu vinavyomchukiza mungu na kuwataka kuwa na hofu
ya Mungu ndani yao.
“Wasanii wengi wanajisahau, swala la kutumia mdawa
ya kulevya ni swala la kimaadili, wengi wetu tunakosa uchaji mungu ndani yetu
na ndio maana tunapopata umaarufu na fedha nyingi hujikuta tukiingia katika
vitendo viovu,” alisema Nantipa.
Msanii huyo anatarajia kuanza kupanda mlima
Kilimajaro kesho asubuhi kutokana na safari hiyo kusitishwa hii leo baada ya
mizigo yao kupotea hivyo kulazimisha Uongozi wa Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro
kuagiza mizigo mingine.
Nantipa katika safari hiyo ataongozana na wanawake
wenzake kutoka Nepal, Tanzania na
Australia kwa lengo la kuhamasisha usawa wa kijinsia, safari iliyodhaminiwa na
shirika la Chakula Duniani (WFP), Cildreach na Really Wild kwa kushirikiana na
hifadhi ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA).
KUTOKA
KUSHOTO NI MWAKILISHI NA MRATIBU WA WFP NCHINI TANZANIA RICHARD RAGAN,
MKUU WA WILAYA YA MOSHI DK.IBRAHIM MSENGI, NA NADIPHA
Akizungumza na Mwanahabari wetu leo asubuhi, Nantipa ambaye
aliwahi kuyjizolea umaarufu katika Tamthilia hiyo inayorushwa kila siku na chombo
Fulani cha Televisheni hapa nchini, alisema ukiachilia mbali ndoto za kupanda
mlima Kilimanjaro mara nyingi amekuwa akitamani kufanya kazi na wasanii wengine
wakongwe barani afrika na moja ya nchi anazozihusudu ni Tanzania.
DC MOSHI AKIZUNGUMZA JAMBO NA NADIPHA |
“Fursa ya kupanda Mlima Kilimanjaro ni moja ya ndoto
zangu kama msanii ndoto ambayo hatimaye kesho (leo) nitaitimiza lakini natamani
sana kuwa msanii mkubwa, natamani kufanya kazi na wasanii wakubwa afrika,
lakini hasa nafikiria kufanya kazi na msanii wa Tanzania na kujifunza Kiswahili,”
alisema Nantipa.
Aidha Msanii huyo mcheshi na mchangamfu alikemea
tabia ya wasanii kujiingiza katika matumizi ya madawa ya kulevya na kuongeza
kuwa inapasa wasanii wajitambua na kutambua dhima iliyoko mbele yao ya
kufundisha jamii na sio kupotoka.
NADIPHA HAKUJIZUIA KUONYESHA FURAHA YAKE
NADIPHA ALIONYESHA KUSHIRIKIANA NA WAANDISHI HABARI MKOA WA KILIMANJARO KUTOKA KUSHOTO SAMUEL SHAO, TADEI MASAWE
NADIPHA NA KHADIJA HAMAD
NADIPHA NA FADHILI ATHUMAN WA BLOGU YA TAIFA LETU
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :