ICF YABORESHA MAZINGIRA YA UWEKEZAJI AFRIKA.
Posted in
No comments
Friday, June 1, 2012
By
danielmjema.blogspot.com
Mtendaji Mkuu wa ICF, Omary Issa amesema kuwa ICF imesaidia kuboresha mfumo wa usajili wa makampuni nchini Rwanda ambapo kwa sasa humchukua mtu siku 2 kusajili biashara tofauti na awali ambapo ilikuwa wakitumia mpaka siku 16 huku gharama zikipungua kutoka dola za Marekani 433 mpaka 25.
Issa alisema kuwa taasisi yake katika kuhakikisha shughuli
za biashara zinafanyika kwa urahisi na ufanisi zaidi imesaidia kuboresha mfumo
wa mahakama nchini Zambia kwenye mahakama 3 na kutoa mafunzo kwa majaji wapya 14
huku nchini Sierra Leone wakifanikiwa kuboresha mfumo wa mahakama ambapo kwa
sasa huchukua miezi miwili tokea kufungua kesi za biashara na kupata uamuzi ambapo
awali ilikuwa inatumia mpaka miaka sita .
alisema kuwa taasisi
hiyo inashirikiana na TRA na Jeshi la
polisi nchini kuboresha utoaji huduma kwa kuhakikisha bidhaa zinazopita nchini (transit
goods) kwenda nchi jirani ya Rwanda zinasafirishwa kwa usalama na haraka kutoka
jijini Dar es Salaam mpaka Rusumo kwenye mpaka wa nchi hizo hivyo kupunguza
gharama za usafirishaji.
afisa wa TRA, Alexander Buchafwe,
MAMLAKA ya mapato nchini (TRA) imeanzisha mfumo wa
kieletroniki wa kufuatilia magari ya mizigo (ECTS) ambao utasaidia kukabiliana
na udanganyifu wa baadhi ya
wafanyabiashara wanaokwepa kodi kwa kuingiza mali nchini kwa madai kuwa zinapita
kuelekea nje ya nchi.
Aidha mfumo huo ambao utawezesha magari hayo kufuatiliwa
moja kwa moja kutoka kwenye ofisi za TRA
huku vifaa hivyo vikutunza taarifa utasaidia kuondoa vizuizi vya kukagua kodi
kwenye barabara ambavyo vilikuwa vikionekana kuwa kero kubwa kwa wenye malori
hasa kutokana na uwingi wake.
Hayo yalisemwa na afisa wa TRA, Alexander Buchafwe,
alipokuwa akitoa maelezo kwenye banda ya
taasisi za serikali za nchi za Afrika zilizonufaika na Taasisi ya kuboresha
uwekezaji Afrika (ICF) ambayo inafanya mkutano wake pili mkubwa wa kimataifa kwenye hoteli ya Naura Spring.
Alisema kuwa mfumo huo ulizinduliwa rasmi Machi 12, mwaka
huu ambapo wamewapa wamiliki wote wa magari ya mizigo muda wa miezi mitatu wawe
wamefunga vifaa hivyo kutoka kwa makampuni sita waliothibitishwa na TRA kwa
ajili ya kufanya kazi ya kuuza na kufunga vifaa hivyo.
Habari na Grace Macha.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :