MAFUNZO KWA WAKAGUZI WA MAHESABU YA SERIKALI KANDA YA KASKAZINI YA WIKI TATU YAMEANZA LEO

Posted in
No comments
Friday, June 1, 2012 By danielmjema.blogspot.com



Mkurugenzi msaidizi wa mafunzo hayo kutoka Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi Felister Kenulembe akizungmza kwenye mafunzo hayo.

Washiriki wa mafunzo hayo.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro Ruth Malisa wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya wiki 3 kwa wakaguzi wa mahesabu ya Serikali  kanda ya kaskazini kutoka mikoa ya Tanga,Kilimanjaro,Arusha na Manyara mafunzo ambayo yameandaliwa na  Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi.
Washiriki wa mafunzo ambao ni wakazi kanda ya kaskazini,wakifuatilia kwa umakini mafunzo.

Hapa Kaimu katibu tawala ruth Malisa akijadiliana jambo na Felister Kenulembe ambaye ni mkurugenzi msaidizi wa mafunzo kutoka ofisi ya taifa ya ukaguzi.

Washiriki ambao ni wakaguzi na viongozi wakiwa kwenye picha ya pamoja
Wakaguzi wa mahesabu ya Serikali nchini wametakiwa  kufanya kazi hiyo kwa umakini kwa kufuata madili na taratibu za kazi ya ukaguzi ikiwa ni pamoja na kutowaonea au kufanya upendeleo kwa wanaowakagua ili kusaidia kuonesha dhamani ya matumizi ya fedha za Sererikali zinazotolewa kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo.
Hayo yalibainishwa jana na Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro Ruth Malisa wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya wiki 3 kwa wakaguzi wa mahesabu ya Serikali  kanda ya kaskazini kutoka mikoa ya Tanga,Kilimanjaro,Arusha na Manyara mafunzo ambayo yameandaliwa na  Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi.
Alisema kuwa taarifa ya wakaguzi inategemewa kwenye shughuli mbalimbali za utafiti pamoja na wataalamu mbalimbali wa serikali katika kuonesha dhamani ya fedha za Serikali,(value for money)hivyo hali hiyo itasaidia wakaguzi kugundua na kuwa na taarifa nzuri za matumizi ya fedha za serikali katika mambo mbalimbali.
“Wakaguzi wa mahesabu wanategemewa katika kutoa maelekezo ya matumizi ya fedha za Seriakali kama jengo,au mradi wowote uliotolewa fedha na Serikali kama kilichofanyika kimeendana na fedha yenyewe,hivyo ni watu muhimu na wanapaswa kupewa mafunzo”Alisema Ruth.
Kwa upande wake Mkurugenzi msaidizi wa mafunzo kutoka Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi Felister Kenulembe alisema kuwa mafunzo hayo yamelengwa kuwaongezea uwezo wakaguzi hususani ni kujifunza mifumo mipya ukaguzi.
Alisema kuwa wakaguzi wanatakiwa kuwa mbele katika kuifahamu mifumo mipya ya ukaguzi ili wasichanganywe na wanaoenda kuwakagua hali itakayosaidia kuandaa taarifa nzuri ambazo zinatonyesha matumizi mazuri ya fedha za Serikali.
“Mifumo ya ukaguzi inabadilika mara kwa mara maana tunatoa vipaumbele kwenye mafunzo ili wakaguzi waweze kuongeza ufanisi kwenye ukaguzi,ambapo leo mafunzo haya pia tumefanyia kwenye jengo letu la wakaguzi  Mkoa wa Kilimanjaro ili kupunguza garama”Alisema  Felister .

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .