KCMC HALI SHWARI

Posted in
No comments
Saturday, June 23, 2012 By danielmjema.blogspot.com


IKIWA ndio siku ambayo chama cha madaktari nchini kilitangaza kufanya mgomo wa nchi nzima, hali imekuwa tofauti katika hospitali ya rufaa ya KCMC, iliyoko mjini Moshi, Mkoani Kilimanjaro kwa madaktari kuendelea na shughuli zao kama kawaida.





Hii inakuja siku moja baada ya mahakama kuu kuamuru madaktari kusitisha mgomo huo kufuatia serikali kutoa pingamizi kwa kuwepo kwa mgomo katika mahakama hiyo hapo jana.

Madaktari hao walikutwa hospitalini hapo wakiendelea na shughuli zao kama kawaida na hata walipoulizwa kuhusu mgomo, mmoja wa madaktari wa hospitalini hapo, ambaye hata hivyo hakuwa tayari kujitambulisha alisema wao wataendelea kutoa huduma kwa wagonjwa hadi pale watakapopata taarifa rasmi kutoka kwa uongozi wa hospitali hiyo.


Juhudi za kuwapata viongozi wa hospitali hiyo kuongelea hali hiyo zilishindikana baada ya kugoma kuzungumza kwa madai kwamba wo sio wazungumzaji wa hospitali hiyo.

Wakiongea katika nyakati tofauti baadhi ya wagonjwa truliofanya nao mahojiano katika wodi mbalimbali za hospitali hiyo, Aranyiaeli Godson na Eva Kornel walikiri kupewa huduma kama kawaida.

 “Hapa kwa kweli hatujashuhudia kitu hicho, wamekuja kama kawaida na tunashukuru tumepewa dawa, tumechekiwa, kwa kweli hamna mgomo hapa ila sijui labda kwa hapo baadae,”alisema Godson

 Hata hivyo pamoja na kuwepo kwa huduma walisema madaktari waliokuja kuwatembelea asubuhi ni wawili tu tofauti na ilivyo kawaida ambapo huwa wanafika zaidi ya wanne kuwajulia hali.




“Ndiyo  tunapewa huduma madaktari tayari wamepita japo sio kawaida, leo wamekuj awawili tu tofauti na kila siku huwa wanakuja hata wanne, watatu na siku nyingine hadi watano,” alisema Eva.






Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .