Lowassa Aongoza Harambee Kuchangia Mpango Wa Elimu Kata Ya Kipawa Jijini Dar Es Salaam
Posted in
No comments
Friday, June 8, 2012
By
danielmjema.blogspot.com
WAZIRI
Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, ameendelea kuwa mstari wa mbele katika
harakati zake za kuchangisha mamilioni ya fedha baada ya kuchangisha Sh.
421,850,000 kwa ajili ya kuboresha Mfuko wa Elimu Kata ya Kipawa katika
Manispaa ya Ilala, jijini Dar es Salaam.
Lowassa,
ambaye ni Mbunge wa Monduli (CCM), aliendesha harambee hiyo juzi katika
hafla iliyofanyika Hoteli ya Kempiski Jijini Dar es Salaam ambapo yeye
mwenyewe alichangia Sh. milioni 10.
Katika
harambee hiyo miongoni mwa kampuni yaliyochangia kiasi kikubwa ni Lions
Club Sh. milioni 70, Home Shopping Center Sh. milioni 22, African
Barrick Gold Dola 10,000, Songas Dola 10,000, Maersk Sea Line ilichangia
Sh. milioni 90, na Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja alichangia
Milioni Sh.10.
Wengine
waliochangia ni madiwani, viongozi wa Chama Cha Mapinduzi, Chadema,
taasisi za watu binafsi na mtu mmoja mmoja ambapo Radio Clauds walitoa
muda wa hewani wa kutangaza mpango huo wenye thamani ya Sh. milioni 12.
Akizungumza
kabla ya kuendesha harambee ya kuchangisha, aliwataka Wakuu wa Wilaya
na Wakurugenzi wa Halmashauri kuendelea kuwahamasisha wananchi kuwekeza
katika kuchangia Sekta ya Elimu.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :