Wanaohama CCM Ni Vinyago - Nape
Posted in
No comments
Friday, June 8, 2012
By
danielmjema.blogspot.com
Katibu
wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Moses Nnauye, amesema wanaokihama
chama hicho kwenda upinzani ni vinyago, ambavyo kamwe haviwezi kumtisha
mchongaji, huku akisisitiza kwamba waasisi wa vyama vya Chadema, NCCR,
CUF, TLP na vinginevyo vyote, ambao walikuwa ndani ya CCM miaka 20
iliyopita, wote hawawezi kuitisha CCM. Nape ametoa kauli hiyo wakati
akiwahutubia wakazi wa Makambako mkoani Njombe.
Hii
ni kauli ya pili ya Nape ndani ya wiki moja, kwani hivi karibuni
alisikika akiwaita hao wanaohama CCM kuwa ni Oil Chafu ambayo haina budi
kuondolewa kwenye injini ili kuweka mpya.
Chanzo ni taarifa za habari za ITV na TBC1
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :