Zitto Kabwe Aiumbua Serikali
Posted in
No comments
Friday, June 8, 2012
By
danielmjema.blogspot.com
IMEDAIWA
kuwa, serikali isingepaswa kuendelea kuomba msaada wowote wa fedha
kutoka nje ya nchi, kama ingetekeleza mapendekezo ya bajeti ya kambi ya
upinzani, yaliyotaka kupunguzwa kwa misamaha ya kodi kufikia asilimia
moja ya pato la taifa, ambayo thamani yake ni sawa na fedha zote za
misaada kutoka nchi wahisani.
Kauli
hiyo, ilitolewa jana na Waziri Kivuli wa Fedha na Uchumi, Zitto Kabwe,
ambaye aliweka wazi kuwa misamaha ya kodi ya asilimia tatu ya pato la
taifa ni sawa na shs trilioni 1.03 ambazo ndizo zinazotolewa na nchi
wafadhili kuisaidia Tanzania.
Zitto
akitangaza mwelekeo wa bajeti yake kwa mwaka ujao wa fedha wa 2012/13,
na kuainisha vipaumbele mbadala, alizidi kuianika serikali na kuitaka
itoe maelezo ya kina ya kwa nini imeshindwa kutekeleza ahadi yake
iliyoitoa bungeni, kwamba misamaha ya kodi itapunguzwa mpaka kufikia
asilimia moja ya pato la taifa.
Zitto
ambaye ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA) alisema kama serikali
ingeyafanyia kazi mapendekezo ya kambi ya upinzani, yangewasaidia
Watanzania kupunguza ukali wa maisha, na kuboresha maisha yao kwa
kiwango kikubwa.
Alitaja
mapendekezo yaliyopendekezwa na kambi ya upinzani, katika bajeti
inayoisha, lakini yakawekwa kapuni na serikali kwa sababu zisizojulikana
kuwa, mbali za misamaha ya kodi ni kupunguza kodi kwenye bidhaa za
mafuta ya petroli na dizeli ili kushusha mfumuko wa bei.
Vipaumbele
vingine vya kambi ya upinzani vilikuwa kufuta mfumo wa posho za vikao
(Sitting allowances) na kupeleka sehemu ya tozo ya ujuzi (Skills
Development levy-SDL) kwenye Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu.
Waziri
huyo kivuli alisema ni mapendekezo mawili tu ya kodi za mafuta ya
petroli na diseli na tozo ya SDL yaliyokubaliwa na kutekelezwa, wakati
pendekezo la misamaha ya kodi lilikubaliwa, lakini serikali imeshindwa
kulitekeleza, ikiwa ni pamoja na kukataliwa kwa pendekezo la kufutilia
mbali posho za vikao, ambalo kambi ya upinzani imerejea wito wake wa
kufutwa kwa mfumo wa posho za vikao (sitting allowances).
Soma zaidi...http://www.freemedia.co.tz
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :