TCRA WATOA SOMO KUHUSU MATAPELI MFUMO WA DIGITALI

Posted in
No comments
Saturday, June 23, 2012 By danielmjema.blogspot.com


MAMLAKA ya mawasiliano Tanzania, TCRA imewataka wananchi kuwa makini na wafanyabiashara matapeli wanaouza vifaa na vyombo vya mawasiliano wakati huu ambapo nchi inafanya mabadiliko katika mawasiliano kutoka katika mfumo wa analogia kwenda mfumo wa digitali.

Kauli hiyo inakuja, kufuatia kuwepo kwa wimbi la wafanyabiashara wanaowatapeli wananchi kwa kuwauzia televisheni zinazotumia mfumo wa analogia kwa kuwadanganya kuwa mitambo hiyo ni ya kidigitali.

Angalizo hilo lilitolewa na mkurugenzi wa matangazo wa TCRA na mwenyekiti wa kamati ya kitaifa ya kuelimisha umma kuhusiana na mabadiliko ya mfumo wa mawasiliano, Habbi Gunze katika mkutano wa kamati hiyo na uongozi wa mkoa wa Kilimanjaro.

“kumekuwa na wafanyabiashara matapeli ambao wamekuwa wakiwalaghai wananchi kwa kuwauzia TV ambazo hazina uwezo wa kupokea mawasilaino ya kidigitali kwa kubandika stika feki zikiopnesha kuwa vyombo hivyo ni ya digitali kumbe sio,” alisema Gunze.

Kuhusu malalamiko ya bei za ving’amuzi, alisema kamati yao imekuwa mstari wa mbele kuishawishi serikali kufuta kodi katika gharama za vin’gamuzi kitu ambacho serikali imetekeleza kwa kufuta kodi hiyo katika bajeti yake ya 2012/13.

Awali akifungua mkutano huo, mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama alisema, mpango wa kubadilisha teknolojia ya analojia inayotumika kwa hivi sasa katika sekta ya utangazaji kwenda teknolojia mpya ya dijitali ni mojawapo ya utekelezaji wa maazimio ya nchi zote wanachama wa umoja wa mawasiliano duniani, ITU.

Gama alitoa wito kwa wananchi wote kuwa wepesi wa kupokea mabadiliko kabla ya desemba 31 mwaka huu ambapo mitambo yote ya mawasilano katika nchi za afrika mashariki zitapozimwa.

“tukubali tu kwa moyo mmoja kubadika kwa kununua vin’gamuzi mapema, kubadilisha vyombo vyetu vya sasa, ili kuepuka usumbufu pale mitambo yote ya mfumo huu wa sasa itakapozimwa,” alisema Gama.

Meneja wa TCRA, kanda ya kaskazini, Annete Mahimbo alisema, kamati hiyo imekuwa ikizunguka nchi nzima kutoa elimu ambapo kwa sasa wanatembelea maeneo ya miji mbalimbali na kuanzia kutokana na muda wanazunguka katika kanda zote lengo likiwa ni kuwafikia watu wengi.

Alisema kazi yao ni kuhakikisha wanakutana na wadau wote wa mawasiliano kabla ya desemba 31 ili kuhakikisha elimu inawafikia watu wengi kwa haraka ili kuepuka usumbufu.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .