Waandamanaji wakaidi polisi Khartoum
Posted in
No comments
Sunday, June 24, 2012
By
danielmjema.blogspot.com
Waandamanaji mjini Khartoum,
Sudan, wametumia matairi waliyoyaasha moto na mawe kuwazuwia polisi
waliojaribu kuzima maandamano dhidi ya serikali kupinga hatua ya
serikali ya kubana matumizi.
Maandamano hayo awali yaliongozwa na wanafunzi, lakini inaarifiwa na wananchi wengine nao wamejiunga nayo.
Polisi wa Sudan wameamrishwa kuchukua hatua haraka kumaliza fujo hizo.
Maandamano hayo yaliyoanza tarehe 16 Juni,
yalichochewa na hatua za serikali za kupambana na msukosuko wa kiuchumi,
uliotokana na Sudan Kusini kusimamisha kusafirisha mafuta yake kwa
kupitia Sudan.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako

0 MAOINI :