WANANCHI WAIGOMEA UONGOZI UJENZI WA BARABARA

Posted in
No comments
Monday, June 18, 2012 By danielmjema.blogspot.com

WANANCHI wa kijiji cha Okaseni, kata ya Uru Kusini, wilaya ya Moshi vijijini, mkoani Kilimanjaro, wameiomba serikali  kuwahimiza viongozi wao katika ngazi za kata na taarafa kuchunguza miradi inayoanzishwa katika vijiji vyao ili kuhakikisha inaendelea ili kuepuka hasara kwa taifa na kuleta manufaa kwa watanzania wote.

Wakizungumza na KIJIWE BLOG katika nyakati tofauti, wananchi hao walilalamikia miradi mingi inayoanzishwa katika vijiji vingi kuishia njiani huku hela na nguvu za wananchi zikiteketea kutokana na uzembe na ufatiliaji mbovu miongoni mwa viongozi na waendeshaji wa miradi.

Wakitolea mfano barabara ya kuanzia kwa eno shop iliyoko katika kata ya Uru kusini hadi katika ofisi ya kijiji cha Okaseni nakusema, awali ilitumia shillingi million 24 fedha zilizotolewa na mfuko wa maendeleo wa jamii, TASAF, ili kutengeneza barabara hiyo, ujenzi ulioanza mwaka 2007 lakini cha kushangaza mpaka sasa mradi huo haujakamilika jambo ambalo limezidi vichwa vyao huku maswali yao yakikosa majibu.

Hali kadhalika, mwaka 2011, chama cha msingi cha KNCU, kilitoa Tsh Milioni 2, kwa ajili ya ujenzi wa barabara hiyo ambapo katika maelezo ni kwamba hele hizo zingetumika kujengea eneo la eno shop hadi ofisi ya kijiji.
Aidha walisema kuwa ili kuonesha kuwa kulikuwa na ubadhirifu wa fedha za umma, ujenzi wa barabara hiyo ilikuwa inafanyika nyakati za usiku ambapo walmkuta mkandarasi aliyepewa dhamana ya kujenga barabara ya kwa eno shop akiendelea na shughuli za ujenzi majira ya saa tatu usiku na wakiwa kaitika harakati za kuhoji ni kwa nini kazi hiyo ifanyike usiku alikuja mwenyekiti wa kitongoji hicho ambaye walimtuhumu kufuja fedha za mradi huo.

Wakijibu tuhuma hizo, uongozi wa kijiji cha okaseni, walikiri kuwepo kwa mradi huo na kusema kwamba shilingi milioni 2 zipo kwenye akaunti ya kijiji na kudai kwamba walimuomba mkandarasi huyo kusaidia kufukia makorongo yaliyopo katika baadhi ya mabarabara ya kijiji kwa gharama zao na kusisitiza kuwa hamna hela ya mradi iliyotumika mpaka sasa.

“Ni kweli kama wanavyosema wananchi barabara ililimwa majira ya jioni, hilo kwa kweli sibishi lakini kitu nisichokubaliana nacho ni kudai kwamba hela zimetumika, nataka niweke wazi kwamba eneo hilo nilimwomba yule mkandarasi anisaidie kufukia makorongo yale tena kwa gharama zangu mwenyewe wakati mikakati ya kujenga barabara ikiendelea,” alisema mwenyekiti wa kitongoji cha okaseni kati, Alphonce Mtaresi, ambaye kipande cha barabara kilicholimwa kipo kitongojini kwake.

Kwa upande wake Diwani wa kata ya Uru kusini, Joseph Komu, alisema hana taarifa ya fedha za mradi wa TASAF wa mwaka 2007 kwani katika kipindi hicho hakuwa madarakani na kuongeza kuwa shilingi milioni 2 za KNCU alizipokea na kukabidhi kwa uongozi wa kijiji ila baada ya kupata tetesi kwamba barabara inajengwa usiku aliandika barua kwa uongozi wa kijiji na kuwapa siku 7 kuanzia  tarehe 12 juni hadi 19 juni mwaka huu wawe wamempa taarifa kamili za mkandarasi huyo na mahali fedha zinazotumika katika ujenzi huo zinapopatikana.

na mwandishi wetu, moshi

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .