Afghanistan yataraji ahadi ya misaada
Posted in
No comments
Saturday, July 7, 2012
By
danielmjema.blogspot.com
Waziri wa Mashauri ya Nchi za
Nje wa Japani, Koichiro Gemba, anasema nchi yake itaahidi dola bilioni
tatu zaidi, kuisaidia Afghanistan.
Alisema hayo kabla ya mkutano mkubwa wa wafadhili wa Afghanistan ambao utafanywa mjini Tokyo Jumalipi.
Bwana Gemba alisema jumla ya dola bilioni 16,
zitaahidiwa kwenye mkutano huo, kuisaidia Afghanistan baada ya NATO
kuondosha majeshi yake.
Hapo awali, Waziri wa Mashauri ya Nchi za Nje wa
Marekani, Hillary Clinton, alitangaza kuwa Marekani inaiona Afghanistan
kuwa rafiki mkubwa na itashirikishwa katika ushirikiano wa kijeshi siku
za mbele
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :