Dunia yaadhimisha miaka 94 ya Mandela
Posted in
No comments
Thursday, July 19, 2012
By
danielmjema.blogspot.com
Rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini Nelson Mandela leo anatimiza miaka 94 tangu alipozaliwa.
Siku ya kuzaliwa kwake pia inaadhimishwa na
Umoja wa Mataifa kutokana na mchango wake katika kuikomboa Afrika Kusini
dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi.
Mandela akiwa na Rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton aliyemtembelea jana |
Na
nchini Afrika Kusini kwenyewe Nelson Mandela, ataadhimisha siku hii na
familia yake na Marafiki huku shughuli mbalimbali zikiandaliwa nchini
humo kama katika kusherehekea siku hii.
Mwandishi wa BBC wa Afrika Kusini, Omar Murtasa,
amesema kuwa Mzee Mandela anaheshimiwa na watu wengi nchini humo,
wakitambua juhudi zake za kupigania Uhuru wa Taifa hilo lilolokuwa
likiongozwa kirasmi na Ubaguzi wa rangi.
gereva la Robben alipokuwa amefungwa |
Ripoti zinasema raia wa nchi hiyo hii leo
watajitolea kufanya kazi ya kuwasaidia wasiojiweza kwa muda wa dakika
sitini na saba kama njia moja ya kuadhimisha siku hii.
Mandela aliachikiliwa huru kutoka gerezani akiwa na umri wa miaka 67.
Mandela alichaguliwa kuwa rais wa Afrika Kusini mwaka wa 1994.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :