MGOMO WA MAGARI WAENDELEA MJINI MOSHI
Posted in
No comments
Monday, July 2, 2012
By
danielmjema.blogspot.com
Na Mary Mosha, Moshi
02 julai
IKIWA ni takribani wiki mbili tu
tangu mji wa moshi ulipokumbwa na adha ya usafiri baada ya madereva wa daladala
kufanya mgomo, mji huo umejikuta ukionja machungu hayo kwa mara nyingine tena
safari hii, ikihusisha mabasi makubwa.
Madereva hao kama ilivyokuwa
kwa wenzao wa daladala, wamegoma kuheshimu ombi la kulipa ushuru wa Tsh. 2000
kama ilivyoainishwa katika tangazo la manispaa ya moshi ya tarehe 18 juni mwaka
huu ikiwataka kulipa ushru wa maegesho ya Tsh. 2000 toka katika ile ya ada ya
kawaida ya Tsh. 1500.
Wakizungumza na gazeti hili,
baadhi ya madereva hao walisema kuwa kilichowapelekea kugomea ushuru huo ni
kitendo cha manispaa kupitisha maamuzi yake bila ya kuwashirikisha waajiri wao
pamoja na wao wenyewe kuhusu ongezeko la ushuru.
Walisema wao kama wadau
wakubwa hawajapokea taarifa zozote za kimaandishi kutoka kwa manispaa
kuwajulisha kuhusu ushuru mpya na kusema kwamba walipokea maelekezo ya kukataa
ushuru huo kutoka kwa waajiri wao kwa madai ya kutokuwa na taarifa ya maandishi
kuhusu ongezeko hilo.
.
Kwa upande wake wakala wa
ushuru aliyeidhinishwa na manispaa, Pinnacle prod. Ltd, alikiri kupokea
maelekezo kuhusu gharama mpya ya ushuru kutoka kwa mwajiri wake ambaye ni
manispaa kitu alichokisimamia lakini cha kushangaza ni madereva kugoma kutii
sheria.
Katibu wa TABOA, Ainea Mrutu
alipoulizwa kuzungumzia mgomo huo, alisema yeye binafsi hakubaliani na kitendo
cha kupandishwa kwa ushuru na kuongeza kuwa kinachoendelea katika kituo hicho
hakiendani na hali halisi ya uchumi katika kituo hicho.
“Unajua swala hili linanishangaza sanma halafu
sijui ni kwea nini manispaa bado inaendelea kutoza ushuru huu wakati katika
kikao cha tarehe 25 tulishakubaliana kumwomba mkuu wa wilaya kukutana na barua
nimeshaandika kinachosubiriwa ni majibu yamkuu wa wilaya, nawashauri manispaa
kusubiri kwanza,” alisema Mrutu.
Kwa upande mwengine, mwenyekiti wa
usalama barabarani mkoa wa Kilimanjaro, Christopher Lyimo, akiongea na gazeti
hili kwa njia ya simu, alisema kuwa yeye kama yeye hayupo katika nafasi ya
kulizungumzia kutokana na swala hilo kwa sasa kuwa katika mikono ya mkuu wa
wilaya ya moshi.
Aidha jeshi la polisi
kikiongozwa na vikosi vya usalama barabarani na kile cha FFU kilifika kituoni
hapo na kuwasambaratisha madereva waliokuwa wamejiandaa kuwafanyia fujo wakala
hao na muda mfupi baadae hali kituoni ilikuwa shwari na madereva waliendelea na
shughulizao kama kawaida ijapokuwa sio wote wealiokubali kulipa ushuru wa
shilingi 2000.
Pia baadhi ya magari yaliondoka bila
kulipa ushuru kitu kilichomlazimu wakala huyo kuandika namba za usajili za
magari hayo kwa ajili ya kuchukuliawa hatua za kisheria.
Kabla ya ongezeko hilo daladala
zilikuwa zinalipa shilingi 1000, mabasi shilingi 1500 na, teksi zililipa
shilingi 200 kama ushuru ya maegesho lakini kwa sasa katika tangazo hilo
lililoanza kufanya kazi tarehe 01 julai mwaka huu, walitakiwa kulipa shilingi
1500 kwa daladala, shilingi 2000 kwa magari makubwa na shilingi 500 kwa teksi.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :