Mubarak kurejeshwa jela
Posted in
No comments
Tuesday, July 17, 2012
By
danielmjema.blogspot.com
Mwendesha mashtaka mkuu nchini Misri, ameaumuru rais wa zamani wa nchi hiyo, Hosni Mubarak kurejeshwa gerezani akisema kuwa hali yake ya afya imeimarika sasa.
Mubarak, mwenye umri wa miaka ,84, alihamishwa kutoka gerezani humo mwezi jana baada ya ripoti za afya yake kuzorota .
Alisemekana
wakati huo kuwa alipatwa na kiharusi mwa mpigo na kuwekwa kwenye
mashine ya kupiga moyo. Ripoti za Mubaraka kupoteza fahamu wakati huo
zilipingwa vikali.
Mwezi Juni , Mubarak alihukumiwa kifungo jela
baada ya kupatikana na hatia ya mauaji ya waandamanaji waliokuwa
waanpinga utawala wake.
Mkuu huyo wa mashtaka, Abdel Maguid Mahmoud
alitoa agizo la kumhamisha rais Mubaraka kutoka hospitali ya kijeshi ya
Maadi hadi katika hospitali ya Tora baada ya afya yake kuimarika.
Naibu wa Mahmoud, Adel al-Saeed, ilisema kuwa
jopo la madaktari lilikuwa hapo awali limesema kuwa afya ya rais huyo wa
zamani iko sawa sasa mradi atumie madawa yake na kwamba kwa mtu mwenye
umri wake hilo ni sawa.
Hata hivyo haikujulikana mara moja lini Mubaraka atarejeshwa tena gerezani.
Aidha mwandishi wa BBC mjini Cairo anasema kuwa taarifa zozote kuhusu afya yake, wamisri wanazichukua kwa shauku kubwa.
Kumekuwa na shauku kubwa kuhusu afya ya Mubarak
wengi wakisema kuwa taarifa zozote kuhusu afya ya Mubarak zinatafsiriwa
kama njama ya yeye kutaka kutolewa gerezani kwa misingi ya afya yake.
Hata hivyo wengi wanajua kuwa huu sio mwisho wa wao kusikia kuhusu sakata hii ya afya ya Mubarak.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :