Watatu wafariki, 13 wajeruhiwa ajalini
Posted in
No comments
Tuesday, July 17, 2012
By
danielmjema.blogspot.com
KAMANDA WA POLISI MKOA WA ARUSHA- LIBERATUS SABAS |
KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, amethibitisha
kutokea kwa vifo vya watu watatu na wengine 13 kujeruhiwa, baada ya
kutokea ajali ya basi dogo la abiria (daladala) katika eneo la Kisongo,
wilayani Arumeru, mkoani Arusha.
Akizungumza mjini hapa jana, Kamanda Sabas alisema ajali hiyo ilitokea juzi, saa sita mchana, baada ya magari mawili kugongana na kusababisha vifo vya watu watatu.
Aliyataja magari yaliyohusika katika ajali hiyo kuwa ni lenye namba za usajili T. 706 BFE aina ya Toyota Hiace, lililokuwa likiendeshwa na Robert Wilbert (32), likitokea Kisongo ambalo liligongana na Toyota Hilux, lenye namba za usajili T 509 AJY, mali ya Shule ya St. Magreth.

Alisema uchunguzi wa awali umeonyesha chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa gari lililobeba abiria aliyejaribu kulipita Land Rover lenye namba za usajili T 696 ACP mali ya Kampuni ya kitalii ya Leopard.
“Watu waliofariki ni Hassan Twaha (30), kondakta wa gari la abiria, mwingine aliyefahamika kwa jina moja la Dachi, mtu wa tatu ni mwanamke anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka kati ya 50-55, ambaye jina lake halijafahamika,” alisema Sabas.
Aliwataja watu waliojeruhiwa kuwa ni askari magereza mwenye namba B.1952 CPL Hussein Ally, Muhamed Juma (30), Festo Damas (24) dereva wa bodaboda, Jabir Abraham, wote wamelazwa katika Hospitali ya Mt. Meru, wakati Robert Wilbert (32), dereva wa daladala alilazwa Hospitali ya Selian.
Alisema majeruhi wengine watano waliokuwa katika ajali hiyo walipatiwa matibabu na kuruhusiwa kuondoka kutokana na hali zao kuendelea vyema.
Na Eliya Mbonea, Arusha
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :