Serikali yakubali kujirekebisha mipaka ya mbuga ya Selous kuruhusu uchimbaji wa madini ya Urani.
Posted in
No comments
Wednesday, July 4, 2012
By
danielmjema.blogspot.com
SERIKALI kwa kushirikiana na kamati ya ulithi wa Dunia ya
UNESCO imekubali ombi la kurekebisha mpaka wa pori la akiba la Selous ili
kuruhusu uchimbaji wa madini ya Urani.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo jijini
Dar es Salaam Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki alisema kamati
hiyo katika kikao chake cha 36 kilichofanyika juni 24 mwaka huu Saint
Petersburg nchini Russia imekubali ombi hilo.
Kagasheki alisema tayari kamati hiyo imetenga eneo la Km 200 kwa
ajili ya uchimbaji wa madini hayo ambayo yataanzwaa kuchimbwa wakati wowote
kuanzia sasa.
“Mimi nimerudi kutoka Russia ambapo nilikwenda kuhudhuria mkutano
huo kwa niaba ya serikali, na kwa mara ya kwanza ombi hilo lilipelekwa kwa
kamati hiyo ya urithi wa Dunia ya UNESCO mwezi julai 2011 ambapo lilijadiliwa
katika kikao chake cha 35 na hatimaye limekubaliwa mwaka huu” alisema
Kagasheki.
Alisema uamuzi huo ulifanyika ili kuruhusu tathimini ya
ardhi mazingira na kukamilisha kwa kutoa muda kwa wataalamu kufika eneo
linarohusika ili kuhakiki taarifa ya tathimini hiyo.
Wakati huohuo Tanzania imekuwa mwenyeji wa mkutano wan chi za
Kusini mwa Afrika utakaofanyika octoba 15 hadi 19 jijini Arusha mwaka huu ukiwa
na lengo la kujadili masuala mbalimbali ya utalii pamoja na uhifadhi katika
hifadhi .
Aidha utajadili changamoto pamoja na mafanikio mbalimbali
yakiwemo masuala ya ulinzi na usalama wa watalii na tanzania imechaguliwa
kutokana na usalama wan chi ulioko hivi sasa na wageni wapatao 300 wanategemea
kuhudhuria mkutano huo.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :