WAKULIMA MWANGA WALALAMIKIA UHARIBIFU WA MAZAO YAO UANAOSABABISHWA NA UKAGUZI WA MAILIASILI

Posted in
No comments
Saturday, July 7, 2012 By danielmjema.blogspot.com

Na Arnold Swai
Mwanga

Wakulima wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro, wameuomba uongozi wa

usalama barabarani mkoa wa Tanga, kukagua usimamizi unaofanywa na
askari polisi katika vizuizi vya barabarani vya  Mombo na Maili
kumi,kutokana na bidhaa zao kuharibiwa vibaya wakati wakikaguliwa
kwenye vituo hivyo

Akizungumza na gazeti hili kwa niaba ya wenzake mwenyekiti wa Mtandao

wa vikundi vidogo Kileo mkoa wa Kilimanjaro, Bakari Mbaga alieleza
kwamba wakulima wanaosafirisha bidhaa zao kwenda jijini Dae-es Salaam
wamekuwa wakiharibiwa mali zao na askari wa kwenye vizuizi hali
inayowasababishia hasara kubwa.

Mbaga alisema kuwa licha ya barabara kuu ya Moshi-Dar-es Salaam  kuwa

na vizuizi vitano vya ukaguzi wa magari, vituo vilivyo mkoa wa Tanga
ambavyo ni Mombo na  Maili Kumi  vimekuwa vikifanya  uharibifu mkubwa
wa mali za wakulima wanaosafirisha  bidhaa zao, kutokana na ukaguaji
mbovu wa askari polisi wa vituo hivyo.

Alisema kuwa askari hao wamekuwa wakikanyaga bidhaa zao, zikiwamo

nyanya, pilipili hoho, mapoja na mikungu ya ndizi kuvunjika  bila
kujali ni mali zinazoharibika kwa muda mfupi, hali inayosababisha
hasara kubwa wanapokuwa wamefika sokoni.

“Kwakweli hali ni mbaya sana kwani wakulima wamejiunga kwenye vikundi

vidogo kwalengo la kupata mtaji wa kusafirisha mazao yao kwenda
sokoni, lakini tumekuwa wakipata hasara zisizo za ulazima kutokana na
askrai katika vizuizi vya ukaguzi kukanya mali hizo na kuziaribu
vibaya, “ alisema Mbaga

Mbaga aliongeza kuwa changamoto nyingine  kubwa wanayoipata ni ukaguzi

huo kuchukua muda mrefu, hali inayosababisha madereva kuendesha magari
kwa mwendo wa kasi kwa lengo la kuwa sokono baada ya kucheleweshwa
kwtka ukaguzi hali inayochangia ajali nyingi kutokea.

Akizungumza kwa njia ya simu na gazeti hili  Kamanda wa polisi mkoa wa

Tanga, Costatine Massawe aliahidi kufuatilia tatizo hilo, na kuagiza
askari hao kutumia busara wakati wa ukaguzi, bila kuaribu mali za
wakulima.

Mwisho.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .