Posted in
No comments
Saturday, July 7, 2012
By
danielmjema.blogspot.com
Na Mary Mosha Moshi
IKIWA ni takribani
wiki mbili tu tangu mji wa moshi ulipokumbwa na adha ya usafiri baada ya
madereva wa daladala kufanya mgomo, mji huo umejikuta ukionja machungu hayo kwa
mara nyingine tena safari hii, ikihusisha mabasi makubwa hali iliyopelekea
polisi wa kutuliza gasia kujikuta wakipigwa na wananchi na madereva wakati
walipokuwa wanajaribu kuleta amani.
Huku maeneo
mengine ya stendi ya magari ya kuelekea Marangu, Sanya juu, Holili, Rombo
na Mwika hapokuwa na magari yaliyoegeshwa huko baadhi ya madedeva
kucheza mpira katika maeneo na wengine wakivunja vunja vibanda vya
wakala waushuru mjini hapo.
Wakizungunza na
NIPASHE, Madereva walisema kuwa kilichowapelekea kugoma
ni ongezeko la ushuru uliopandisha na manispaa
Moshi bila kuwashirikisha wao kama wadau wao kutoka Tsh 1000 hadi 2000 kwa magari makubwa na kutoka
500 hadi 1500 kwa Haisi.
Walisema wao kama
wadau wakubwa hawajapokea taarifa zozote za kimaandishi kutoka kwa manispaa
kuwajulisha kuhusu ushuru mpya na kusema kwamba walipokea maelekezo ya kukataa
ushuru huo kutoka kwa waajiri wao kwa madai ya kutokuwa na taarifa ya maandishi
kuhusu ongezeko hilo..
““Hapa sisi kwa
kweli hatuelewi hii Manispaa inaendeshwaje , maana haingii akilini
kwa kwa mtu yoyote Yule haya mambo wanayoyafanya bila
kutushirikisha wadau katika maamuzi yao, hapo wanajua hali ya
uchumi ni mbaya, je wanadhani madereva hawana familia, watoto wanaosoma?
Hatufanyi kazi na wao waje waendeshe magari na kupata hizo fedha
wanazotaka ,hata kama mji ni wao!” walisema madereva.
aidha
waliongeza kuwa endapo Manispaa ya Moshi haitasikia kilio chao nakushusha
ushuru wako tayari kuegesha magari yao nyumbani kwani hayawezi kuharibika na
hawako tayari kuumia kwaajili yakunufaisha halmashauri ya Manispaa inayotaka
kupandisha mapato.
Baraza la
madiwani la manispaa ya Moshi lililokaa juzi lilisema kuwa ushuru uliopangwa wa
Sh. 1,500 kwa magari madogo na Sh. 2,000 kwa magari makubwa utabaki kuwa
hapohapo kwani ni sheria na imeshapitishwa kutokana na kwamba Halmashauri
inaendeshwa kwa mapato na kwa atakayeona hawezi kulipa ushuru huo akapaki gari
lake nyumbani.
Kufuatia
kuwepo kwa hali hiyo kiliitishwa kikao cha dharura kilichohusisha kamati ya
ulinzi na usalama wilaya,ofisi ya mkurugenzi manispaa ya Moshi, Sumatra, wadau
wa usafirishaji pamoja na viongozi wa chama cha wamiliki wa mabasi na
usafirishaji mkoani Kilimanjaro (AKIBOA).
Aklizungumza
kaimu mkuu wa mkoa wa Kilimnjaro ambaye ni mkuu wa wilaya ya Moshi Dkt. Ibrahim
Msengi alitoa maombi kwa mamlaka husika kusogeza muda wa utekelezaji wa sheria
hiyo ambayo ilianzwa kutekelezwa rasmi toka julai mosi ili kutoa nafasi ya
majadiliano.
Aidha Dkt.
Aliwataka wasafirishaji kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa amani na utulivu
kwa kuzingatia sheria ikiwa ni pamoja na kuepuka vurugu.
Naye Kaimu
mkurugenzi wa manispaa ya Moshi Dkt. Christopher Mtamakaya alisema sheria ya
mabadiliko ya ushuru kutoka Sh. 1000 hadi 1,500 na 2,000 ulipitia mchakato wote ikiwa ni
pamoja na kuwashirikisha wadau wa usafirishaji na kwamba kwa sasa hawawezi
kubadilishwa sheria hadi pale ambapo maombi yaliyotolewa na kaimu mkuu wa mkoa
yatakubalika.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :